loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mourinho: Sikupewa muda Manchester United

KOCHA wa Tottenham, Jose Mourinho amefunguka na kusema hakupewa muda wa kutosha wa kutekeleza mipango yake akiwa kocha wa Manchester United.

Mourinho ana amini anaweza kudumu Spurs kwa muda mrefu zaidi huku akidhani kuwa hakupewa wa kutosha kukamilisha mipango yake kwenye klabu ya Manchester United.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea ambaye hivi karibuni aliadhimisha kipindi cha mwaka mmoja tangu alipopewa jukumu la kuinoa Spurs akichukua nafasi ya  Mauricio Pochettino msimu uliopita, ameipaisha timu yake hiyo mpya msimu huu.

Spurs ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya mabao na mabingwa watetezi Liverpool.

Baada ya kupata mafanikio ya haraka katika klabu mbalimbali alizowahi kufundisha, kocha huyo kutoka Ureno alisema alikuwa na mipango ya muda mrefu katika klabu ya Manchester United lakini ilikatishwa katika muda mfupi kabla ya kuitekeleza.

"Wakati fulani katika maisha yangu ya ukocha kwa ukubwa wa klabu nilizowahi kufundisha hatukuhitaji muda mrefu kupata mafanikio." 

"Tulifanya hivyo nikiwa na Porto, Inter Milan, Real Madrid, Chelsea. Tulipata mafanikio bila ya kutumia muda mrefu na pia shauku yangu ya kujaribu vitu tofauti na shauku yangu ya kutamani kwenda nchi tofauti na kujaribu kushinda makombe na kupata uzoefu tofauti.”

"Klabu moja ambayo nilidhani nilihitaji muda na sikupewa ilikuwa Manchester United kwa sababu nilidhani nilikuwa katikati ya mipango, lakini nilijifunza mapema kuheshima maamuzi ambayo nilifanya nikiwa United.”

"Tulifanya kile tulichofanya, tulifanya kile ambacho ni rahisi kufanya na tulisonga mbele. Nina furaha na wao wana furaha na tuna uhusiano mzuri kitu ambacho najivunia wakati wote kusema kwamba wakati naondoka kwenye klabu fulani naacha mahusiano mazuri na kila mmoja na United ni mfano mmojawapo katika hilo," alisema.

Mourinho amekuwa kocha kwa zaidi ya miaka 20 akipata mafanikio makubwa kila alipokwenda na sasa ana miaka 57 na amesema anaweza akadumu Spurs kwa muda mrefu.

KOCHA Atalanta Gian Piero Gasperini amesema mwamuzi aliharibu ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi