loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Matukio awafunda wasanii

ALIYEKUWA mshindi wa taji la Vyuo na Vyuo vya elimu ya juu (Mr University) Tanzania mwaka 2002  Matukio Chuma, amewashauri wasanii kuepuka maisha bandia kwani huwaumbua wengi wanapougua au kufariki dunia.

Matukio ambaye pia ni mshindi wa pili wa ‘Mr University World ‘Mwaka 2003, alisema hayo kwenye uzinduzi wa toleo la pili la kitabu chake kiitwacho: ‘Matukio; Nimejifunza na Naendelea Kujifunza’ uliofanyika Dar es Salaam juzi.

Alisema baadhi ya wasanii wanatumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kupiga picha na kujitangaza ili waonekane wanaishi maisha ya juu, tofauti na uhalisia jambo linalowaumbua baadaye ukweli unapobainika.

“Lazima Watanzanai wote tuwe makini na mitandao ya kijamii  maana wakati mwingine inawafanya baadhi ya watu kutengeneza na kuishi maisha ambayo si yao halisi, yaani wanajitahidi kuishi maiasha ya ndoto, ya kufikirika na ya kudanganya tofauti na uhalisia” alisema.

 “Mfano mzuri ni baadhi ya wasanii wanaoishi maisha bandia hata kwa kuazima magari au kutumia pesa wanazopata kutaka waonekana wana maisha ya juu, wengine kupanga nyumba za kifahari ili waonekane lakini kumbe wanaisha maisha yasiyo halisi na watu wanawashangaa ukweli wa maisha yao unapobainika hasa wanapougua au kufariki dunia.”

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ...

foto
Mwandishi: Na Joseph Sabinus

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi