loader
Dstv Habarileo Mobile
Picha

Operesheni kuondoa walimu wa kigeni yaja

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako Profesa Ndalichako amesema serikali itafanya hivi karibuni operesheni ya kukagua taasisi za elimu, zinazoajiri walimu kutoka nje bila kufuata taratibu na sheria za nchini.

Amesema mpaka sasa wana taarifa ya shule tano, ambazo zinalalamikiwa kuajiri walimu wa kigeni bila kufuata taratibu na sheria za nchi za ajira.

Amesema kuwa kwa sasa wanafanya uchunguzi shule hizo.

Alisema hayo wakati akifunga Mkutano wa 15 wa Chama cha Wakuu wa Shule za Sekondari za Umma na Binafsi Tanzania (TAHOSSA).

Profesa Ndalichako alisema kwa sasa baadhi ya shule binafsi za msingi na sekondari na taasisi za elimu vikiwamo vyuo vya juu, zimekuwa kichaka cha kuweka watu bila kuzingatia sheria za nchini.

" Baadhi ya shule binafsi zimekuwa zinakiuka masharti ya ajira kwa kuajiri walimu wa kigeni bila kufuata taratibu za ajira za nchi.

"Najua hili sio lenu (wakuu wa shule) ni la wenye shule, lakini nalisema kwa sababu sheria inakata mtu akija kuishi na kufanya kazi bila kibali, unapaswa kutoa taarifa.

"Nimeshazungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia ajira, Mheshimiwa Jenista Mhagama  na bahati nzuri Rais John Magufuli amelizungumzia hili wakati wa kutuapisha kwa kutaka masuala ya ajira yaende vizuri, kwa hiyo nitampa ushirikiano katika hili” alisema.

Profesa Ndalichako aliongeza: "kwa hiyo kama mlikuwa mnaona taasisi za elimu ni kichaka, basi anzeni kuchoma moto vichaka vyenu, tunakuja huko kukagua, tutafanya utafiti kujiridhisha kama wanaofanya kazi kwenye taasisi za elimu ikiwa ni pamoja na vyuo vikuu, elimu  ya kati, shule za msingi na sekondari wanafuata taratibu.

"Hivyo wakuu wa shule anzeni kutoa taarifa, lazima sheria za nchi zifuatwe, na msiwe na wasiwasi na kutishwa na wamiliki wa shule, tutawalinda wote wanaotupa taarifa" alisema.

Aidha, Profesa Ndalichako alisema wakuu wa shule wasiojiongeza, hawatavumiliwa tena.

Aliwapongeza wakuu wa shule kwa juhudi zao katika utoaji elimu, jambo ambalo limefanya ufaulu kuongezeka kila mwaka.

" Endeleeni kuchapa kazi na msikubali wachache wakawaharibia" alisema.

Katia hatua nyingine, Profesa ndalichako alitaka shule binafsi kufuata taratibu na masharti ya uanzishwaji wa shule.

"Umejitokeza mtindo kwa shule ambazo zimesajiliwa kuwa za kutwa na kujenga majengo na kuibadili kuwa ya bweni, kama unataka kuifanya ya bweni fuata na zingatia vigezo na masharti yaliyopo” alisema.

Profesa Ndalichako aliwataka wakuu wa shule, kuhakikisha ulinzi na usalama wa shule ; na kushirikiana na ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kukagua miundombinu ya umeme ili kuondokana na ajali za moto, zinazotokea mara kwa mara.

Pia Profesa alitaka wakuu wa shule kusimamia suala la nidhamu shuleni kuanzia kwao, walimu na wanafunzi.

" Tusimamie nidhamu na maadili ya walimu na  wanafunzi, wanafunzi wanatakiwa kuishi kwa kuzingatia maadili na mila za Kitanzania, tuhimize uzalendo na kuimba nyimbo za uzalendo.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

2 Comments

 • avatar
  Filbert Mahay.
  24/12/2020

  Big up!. It is a good program to observe and see that wether school obey principles and procedures as enacted by government or not. This help to improve academic matters.

 • avatar
  MUKOYA AYWAH
  28/12/2020

  Habari kamilifu na yakupendeza. Heko Mwanahabari Anastazia Anyimike Kwa uandishi sahihi. Ila isiwe ni kuvuruga walimu wageni jinsi Waziri anavyosema.. itakuwa ni kinyume na wimbo wa "Tanzania Tanzania nakupenda" , wimbo wa Taifa na wimbo wa Jumuia ya Afrika Mashariki. Waziri na wenzake wawe makini mno maana uamuzi hafifu ukifanywa, uchumi utayumba na utakuwa mzigo Kwa WaTanzania. Shukran #HabariLeo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi