loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kalemani akataa ombi la kuzima umeme kwa wiki

WAZIRI wa Nishati, Dk Merdad Kalemani amekataa ombi la wakandarasi kuzima umeme kwa wiki moja na kuwapa siku moja ili wabadilishe nguzo katika Kituo cha Zuzu kwa ajili ya kuanza kutumia umeme wa kilovoti 220 badala ya kilovoti 48.

Amelipongeza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kukamilisha ujenzi wa mradi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha kilovoti 220 kilichopo Zuzu Dodoma kwa wakati, ikiwa ni siku nane kabla ya muda uliopangwa. Awali umeme uliokuwa ukizalishwa katika kituo hicho ni wa kilovoti 48.

Kalemani alisema akiwa ziarani kukagua utekelezaji wa mradi wa vituo vya kupokea na kupoza umeme vya Zuzu jijini hapa.

Septemba, mwaka huu, waziri huyo alifanya ziara ya ukaguzi katika kituo hicho na kutoa maagizo kwa wakandarasi na Tanesco kukamilisha mradi huo ifikapo mwisho wa mwezi huu, lakini wao wamekamlisha siku nane kabla ya mwisho wa mwezi.

Dk Kalemani alikataa ombi la wakandarasi la kuzima umeme kwa wiki moja ili kubadilisha nguzo na kuruhusu wateja ikiwemo Mji wa Serikali na Ikulu kutumia umeme huo wa kilovoti 220.

Alisema hayuko tayari kuruhusu wateja kukosa umeme kwa wiki moja, hivyo watumie siku moja kufanya kazi hiyo ili wateja waendelee kupata huduma hiyo wakati wote na kuendelea na shughuli za uzalishaji mali hususani kipindi hiki cha sikukuu.

Kituo cha Zuzu kilianza kujengwa mkoani Dodoma miaka mitatu iliyopita kutokana na mahitaji ya Mji wa Dodoma kuongezeka hadi kufikia megawati 48 sawa na uwezo wa kituo kilichokuwepo awali.

Kalemani alisema kukamilika kwa kituo cha Zuzu kunalifanya Jiji la Dodoma kuwa na megawati 248, umeme ambao ni mwingi na utavutia wawekezaji.

Alisema kuwa kitakapo kamilika kituo cha kilovolti 400, Jiji la Dodoma litakuwa na jumla ya megawati 600, huku megawati 400 zikitoka kwenye kituo cha kilovolti 400.

Alisema mradi huo umegharimu Dola za  Marekani Sh milioni 48 na utahusisha mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara.

Awali, Mratibu wa mradi huo Peter Kigadya alisema mradi wa kilovoti 220 umekamilika na tayari meshaanza kutumika na ifikapo Januari 8, mwakani wataunganisha laini ya mji wa serikali na maeneo mengine.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

1 Comments

  • avatar
    Frank Nkingwa Myette
    26/12/2020

    Tunamuomba waziri atuambie kuhusu nguzo za umeme je zinauzwa au haziuzwi maana wilaya ya kishapu kata ya uchunga nguzo tumeambiwa tulipie 250,000. Hata shinyanga mjini mita 18 nimeambiwa nilipie nguzo hatuelewi kati ya waziri huyu na wafanyakazi wa shirika la umeme nani yuko sahihi kama haitoshi tunaomba aje shinyanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi