loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Klopp akanusha Salah kuondoka

BOSI wa Liverpool Jurgen Klopp amekanusha madai ya Mohamed Salah kwamba anaweza kuondoka klabuni hapo baada ya mshambuliaji huyo kutokataa madai ya kuhamia Barcelona au Real Madrid siku zijazo. 

Akizungumza kwenye mahojiano na AS, Salah alisema hatima yake iko mikononi mwa klabu. Lakini Klopp alisema mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri ana ari kubwa Anfield.

"Hatujazungumza [kuhusu mkataba]," Klopp alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu mechi ya Ligi Kuu kati ya Liverpool na  West Bromwich Albion inayotarajiwa kuchezwa kesho. 

"Mo yupo katika hali nzuri kwa sasa na hilo ndilo muhimu zaidi unaweza kumuona akicheka sana.”
"Mengine ni mazuri kwenu kuandika lakini hakuna ukweli.”

Salah aliingia uwanjani akitokea benchi na kuchangia mabao mawili na kutoa pasi ya bao katika ushindi wa Liverpool wa mabao 7-0 dhidi ya Crystal Palace Jumamosi iliyopita.
Klopp alisema matokeo hayo yameondoa fedheha ya kufungwa mabao 7-2 waliyopata kwa Aston Villa mwanzoni mwa msimu huu. 

"7-0 ni namba ambayo hamtaiona,” aliongeza Klopp. "Baada ya mechi na Palace fikra zangu tumefuta yale ya Villa.Hatuihesabu sana mechi ile ili tusonge mbele.”

KOCHA Atalanta Gian Piero Gasperini amesema mwamuzi aliharibu ...

foto
Mwandishi: LIVERPOOL, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi