loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jesus, Walker, wakutwa na Corona

MSHAMBULIAJI wa Manchester City Gabriel Jesus na beki Kyle Walker wamekutwa na Corona. Wachezaji hao na maofisa wawili watalazimika kuwa karantini kwa mujibu wa taratibu za serikali.

City haitakuwa na wachezaji hao kwenye mechi zake za Ligi Kuu dhidi ya Newcastle United iliyotarajiwa kuchezwa jana na dhidi ya Everton kesho na dhidi ya Chelsea Januari 3.

Jesus hakuna shaka nafasi yake itachukuliwa na Sergio Aguero aliyerudi uwanjani baada ya kupoba goti, Jumanne ya wiki hii alicheza kwa dakika 16.

Mshambuliaji wa Brazil Jesus, 23 amefunga mabao manne msimu huu lakini alikosekana kutokana na kuwa majeruhi kwa mwezi mzima huku mchezaji mwenye umri wa miaka 30 Walker hajawahi kucheza katika kikosi cha sasa cha Pep Guardiola.

Beki wa kulia wa England Walker aliomba radhi Mei mwaka huu kwa kuvunja sheria za karantini za kujinga na Corona mara mbili.

Manchester City kwa sasa ipo nyuma kwa pointi nane nyuma ya vinara wa Ligi Kuu Liverpool ikiwa na mechi mkononi.

KOCHA Atalanta Gian Piero Gasperini amesema mwamuzi aliharibu ...

foto
Mwandishi: MANCHESTER, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi