loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Klopp ashangaa wanaotaka kuondoka Liver

J URGEN Klopp amesema haelewi kwanini mchezaji atake kuondoka Liverpool, lakini hamlazimishi yeyote kubaki kama anataka kuondoka klabuni hapo.

Mohamed Salah amekuwa akizungumzwa kuhusu kuhamia Real Madrid, Barcelona na Paris Saint-Germain.

Mbali na hilo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ameacha milango wazi kwa siku zijazo kwenda Hispania huku akielezea kusikitishwa kwake kwa kutokuwa nahodha wa Liverpool katika mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Midtjylland.

Goal inaweza kuthibitisha kuwa Reds imempa ofay a mkataba mpya Salah huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika 2023 na mshambuliaji wa Misri amesema kwa sasa ameelekeza nguvu zake kwenye kuvunja rekodi Anfield.

Tetesi zinasema huenda dirisha la usajili la Januari linaweza kuwa na maamuzi lakini Klopp ambaye alizungumzia pia suala ya Salah kutaka unanodha anaamini nyota huyo wa zamani wa Roma anakila kitu anachokihitaji Merseyside.

“Tutatizama kitu kingine kama tutataka, lakini kwangu, sababu pekee ya kuondoka Liverpool kwa sasa ni hali ya hewa,” alisema Klopp akitabasamu. “Sababu gani nyingine itakuwa?

Hii ni moja ya klabu kubwa duniani, tunalipa fedha labda pengine sio klabu nzuri zaidi duniani, lakini tunalipa vizuri, tuna uwanja mzuri na mashabiki wazuri duniani kote. R

angi yetu ni nyekundu ambayo ni nzuri kwa hiyo sababu ya kuondoka ni nini?”

“Huwezi kulazimisha mtu abaki, hatuwezi ni suala la muda tu, wakati sahihi tumefanya mabadiliko na kusajili wachezaji na kama mchezaji anataka kuondoka hatuwezi kumlazimisha, ni kwamba tu sielewi kwanini mchezaji atake kuondoka.”

Liverpool ipo kwenye kiwango kizuri na ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa ya kutetea tena taji. Kikosi hicho cha Klopp baada ya mapumziko ya Krismas leo kitakuwa nyumbani kuikaribisha West Brom.

Salah alipumzishwa katika mechi ya mwisho ya Liverpool dhidi ya Crystal Palace, lakini aliingia akitokea benchi na kufunga mara mbili na pasi moja ya bao katika ushindi wa Mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus kulia na beki Kyle Walker. mabao 7-0.

KOCHA Atalanta Gian Piero Gasperini amesema mwamuzi aliharibu ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi