loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Miujiza ya mafuta ya nazi na mdalisini katika nywele

NYWELE zenye afya hutokana na kutunzwa. Kuna njia nyingi unaweza kutumia kutunza nywele zako zikiwemo njia za asili kabisa na kuzifanya nywele kuwa zenye nguvu na afya.

Mafuta ya nazi na ya mdalasini, hivi vitu vina uwezo mkubwa wa kudumisha unyevu wa nywele zako na kuzuia kukatika nywele.

Sifa ya mdalasini ni kuzifanya nywele zako kukua na kuimarisha vifuko vya nywele kwa kuchochea mzunguko wa damu kichwani. Lakini pia kama unapenda nywele ndefu na zenye nguvu, mchanganyiko wa mafuta ya nazi na mdalasini ni suluhu mojawapo. -

Kwanza changanya kijiko kimoja cha mafuta ya nazi na kijiko moja cha mdalasini kwenye bakuli. - Gawanya nywele zako kuelekea chini na anza kupaka mchanganyiko kwenye ngozi ya kichwa. -

Tumia ncha za vidole vyako kwa kusugua mchanganyiko kwenye kichwa chako. - Halafu funika nywele zako kwa kitambaa na kofia ya kuogea kwa dakika 30 hadi 45.

Kisha osha nywele kwa kutumia shampuu ya kawaida.

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi