loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mmecheza kizembe, Lampard awaka

KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard amewajia juu wachezaji wake baada ya kufungwa mabao 3-1 na Arsenal juzi, akisema kucheza kwao kizembe kumeigharimu timu.

Mkwaju wa penalti wa Alexandre Lacazette na mabao ya Granit Xhaka na Bukayo Saka yaliisaidia Arsenal iliyosheheni vijana kupata ushindi wa kwanza baada ya takriban miezi miwili.

"Ilikuwa nafasi ya kushika nafasi ya pili dhidi ya timu iliyokuwa kwenye wakati mgumu,” alisema Lampard ambaye kikosi chake kimeporomoka hadi nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi.

"Ilikuwa ni ama ufanye ugumu kwao au uwafungulie na tulifanya hivyo kuanzia dakika ya kwanza na kuendelea kwa dakika 45. Ni uzembe kusababisha penalti ugenini na uzembe kusababisha adhabu ugenini (bao lililofungwa na Xhaka)."

Chelsea ilibadilika katika kipindi cha pili na kufunga bao la kufitia machozi katika dakika ya 85 kupitia kwa Tammy Abraham na kufanya matokeo kusomeka 3-1 kabla Jorginho hajakosa penalti.

"Tulipambana lakini katika kipindi cha kwanza tulijipa wenyewe kazi kubwa ya kufanya, nitabeba lawana za nje lakini wachezaji pia wanatakiwa kubeba lawama.”

"Ujumbe ulikuwa wazi, Arsenal ni timu hatari unapokuwa ugenini na kucheza kwa silimia 60 au 70 kisha hushindi mechi za Ligi Kuu,” alisema Lampard.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alisema amefurahia ushindi huo ulioipeleka timu yake kupanda hadi nafasi ya 14.

"Hakuna zuri zaidi ya kushinda debi ya London dhidi ya Chelsea kwenye ‘Boxing Day’." "Nina imani hii ni sehemu ya kurudi, najua wanaweza kucheza kwa kiwango hiki.”

"Acha tuendelee bado tuna mambo mengi ya kuyabadilisha,” alisema.
 

KOCHA Atalanta Gian Piero Gasperini amesema mwamuzi aliharibu ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi