loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Arteta shangwe  kama zote

KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amesema timu yake iliwaangusha mashabiki kwa wiki nyingi kabla ya kuwafurahisha kwa ushindi wa mabao 3-1 kwenye Ligi Kuu juzi dhidi ya Chelsea.

The Gunners imeshinda mechi ya kwanza ya ligi nyumbani tangu Oktoba mwaka huu kwa mabao ya Alexandre Lacazette, Granit Xhaka na Bukayo Saka yaliyowaweka mbele kwa 3-0 kabla ya bao la dakika za majeruhi la Tammy Abraham.

Arsenal haikushinda katika mechi saba zilizopita kwenye ligi ikipoteza tano kati ya hizo. Akizungumza baada ya mechi Arteta alisema matokeo hayo yanawafanya kufurahia lakini kikosi chake kiliwachanganya mashabiki kwa kukosa ushindi katika mechi zilizopita.

"Matokeo ni jambo kubwa leo (juzi) tumekosa bahati na kuchanganya watu kwa matokeo yetu, tulihitaji ushindi huu, tumewachanganya mashabiki wetu kwa matokeo mabaya kwa wiki nane zilizopita kwa hiyo hii ni siku kubwa kwetu.”

"Kuanzia filimbi ya kwanza unaweza kuona nguvu iliyokuwapo na ari ya kutaka ushindi.”
"Ari waliyokuwa nayo wachezaji kabla ya mechi ilikuwa kubwa walihitaji ushindi hasa, ninafuraha kwa ajili ya wachezaji wangu na mashabiki wetu kwani tumewaangusha mara nyingi hivyo ni siku nzuri kuwapa kitu.”

"Tulipopata penalti sikuamini, huu ndio mchezo wa soka, mara zote utakushangaza,” alisema Arteta.

Arteta an aamini mechi hiyo itairudisha Arsenal kwenye mstari msimu huu.

“Nina imani hii ni pointi ya kuanzia najua wanaweza kucheza kwa kiwango hiki, tunajua Chelsea ilivyo nzuri lakini tukio kubwa kweye mechi ni kwamba tulikuwa timu bora.”

"Majeruhi, Covid, kucheza na wachezaji 10 unaanza kufikiri unavyohitaji kushinda mechi.”

"Ni nzuri kuwapa kitu mashabiki kwasababu unaweza kufikiri jinsi walivyokatishwa tamaa, tumeanza vizuri na kutawala mchezo, hilo linaifanya timu kujiamini,” alisema.

KOCHA Atalanta Gian Piero Gasperini amesema mwamuzi aliharibu ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi