loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Messi sasa atamani kucheza Marekani

NAHODHA wa Barcelona, Lionel Messi amesema ana imani siku moja atacheza Marekani lakini hana hakika na hatima yake atakapomaliza mkataba wake Barca Juni mwakani.

Mshambuliaji huyo wa Argentina 33 anaweza kuanza mazungumzo na klabu nyingine Januari. Tetesi juu ya hatima yake zimekuwa zikizagaa tangu alipoomba uhamisho Agosti.

“Sijajua bado nitakachofanya. Nitasubiri mpaka msimu uishe, ningependa kucheza Marekani ili nipate uzoefu wa maisha na ligi ya kule, lakini ukirudi Barcelona ni jambo lile lile.”

“Kwa sasa jambo muhimu ni kuelekeza nguvu kwa timu imalize msimu vizuri kujaribu kutwaa mataji na si kingine,” Messi alikiambia kituo cha runinga cha Channel La Sexta cha Hispania.

Barcelona ambayo haikutwaa taji lolote msimu uliopita ipo nafasi ya tano kwenye msimamo wa La Liga baada ya kuanza vibaya kampeni zake za ligi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 33.

Tangu alipojiunga nayo akiwa na umri wa miaka 13, Messi amekuwa mfungaji mwenye rekodi klabuni hapo, akishinda mataji 10 ya La Liga, manne ya Ligi ya Mabingwa na kutwaa tuzo ya Ballon d’Or mara sita.

Maombi yake ya kuomba kuondoka Barcelona kufuatia kutofautiana na Rais wa klabu, Josep Maria Bartomeu aliyejiuzulu Oktoba yamechanganya wengi.

“Ni wakati mgumu kwa klabu, kwa kila mmoja, lakini wote walio ndani ya klabu wanajua jinsi gani hali ilivyokuwa mbaya, mambo ni mabaya na itakuwa ngumu klabu kurejea ilipokuwa,” alisema.

KOCHA Atalanta Gian Piero Gasperini amesema mwamuzi aliharibu ...

foto
Mwandishi: BARCELONA, Hispania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi