FRANK Lampard amesema Chelsea haina nafasi ya kutwaa taji la Ligi Kuu na kutaka yafanyike mabadiliko katika mechi ijayo dhidi ya Aston Villa.
Chelsea ilifungwa mabao 3-1 na Arsenal kwenye ‘Boxing Day’ ikiwa ni kipigo cha tatu kati ya mechi nne za Ligi Kuu ilizocheza na kushuhudia ikiporomoka hadi nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi.
Lampard amelalamika kuhusu ratiba ya Chelsea akisema haiwezekani timu moja icheze mechi mbili ndani ya saa 48 na aliacha nyota wake kadhaa katika mechi ya uwanja wa Emirates ili aimudu ratiba.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alikuwa mmoja wa waliosema Chelsea ina nafasi ya kutoa upinzani kwenye kuwania taji msimu huu, lakini Lampard amesema maoni hayo yanazihusu timu zinazopewa nafasi kubwa lakini si timu yake licha ya kutumia zaidi ya pauni milioni 220 msimu huu.
“Kutakuwa na baadhi ya mabadiliko dhidi ya Aston Villa (ilitarajiwa kuchezwa jana), “ alisema Lampard