loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kuwasilisha Namba ya Mlipakodi TRA mwisho kesho

MAMLAKA ya Mapato Tanzania imehimiza waajiri wahakikishe waajiriwa wote nchini, wamewasilisha Namba ya Mlipakodi (TIN) kwenye Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ifi kapo kesho Desemba 31.

Akizungumza na HabariLEO jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema mamlaka hiyo ilitoa muda wa miezi mitano, kuanzia Agosti mwaka huu hadi Desemba 31, mwaka huu ili waajiriwa wawasilishe TIN hizo.

“Tulitoa muda mrefu kuanzia Agosti mwaka huu hadi Disemba 31 ili waajiriwa wote wawasilishe TIN Namba zao kwa waajiri zitufikie, tunashukuru mwitikio ni mkubwa wengi wamewasilisha ila bado wapo ambao hawajatekeleza, tunawahimiza watekeleza ndani ya muda uliopangwa,”alisema Kayombo.

Alisema baada ya muda huo kwisha, hakutakuwa na nyongeza ya muda kwa sababu upatikanaji wa TIN Namba ni rahisi na mwajiriwa anaweza kuipata ndani ya dakika chache tangu ajisajili kwenye mtandao wa TRA kuomba kupewa namba hiyo na kuiwasilisha kwa mtandao pia.

“Zoezi hili ni la watumishi wote nchini walioajiriwa popote pale wawasilishe TIN kwa mwajiri, litadumu hadi Desemba 31,2020, kwa hiyo waajiri wote tumeshawaagiza wahakikishe wafanyakazi wao wamewasilisha TIN zao”alisema Kayombo na kuongeza: “Kwa kipindi hiki tumerahisisha kwa kila mtu kutumia mtandao ili kuondoa usumbufu kwa mtu yeyote kufika ofisi za TRA”.

Kayombo aliwataka wananchi hasa wale wanaokwenda maeneo ya burudani katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka, kudai risiti za kielektroniki (EFD) wapatapo huduma. Alisema kufanya hivyo ni kuhakikisha kodi stahiki zinalipwa, kwa kuwa wapo wachache ambao hukwepa kulipa kodi kwa visingizio mbalimbali.

Alisema kodi hizo zinahitajika ili zitumike kwa maendeleo ya wananchi. Kayombo pia alihimiza wanaolipa kodi za mapato kipindi cha awamu ya nne, kufanya hivyo ili kuepuka adhabu.

Alisisitiza pia ulipaji wa kodi za majengo kuwa unaendelea na kwamba nyumba ya kawaida ni Sh 10,000 na kwa ghorofa, sakafu moja ni Sh 50,000. “TRA tunahimiza hata wakati huu wa msimu wa sikukuu, wananchi waendelee kulipa kodi mbalimbali na pia tunawahimiza wale walio na mashine za EFD wakaziboreshe ili zitoe risiti za EFD zenye nembo ya QR CODE na mwisho wa kuboresha mashine hizo ni Januari 7, mwaka 2021”alisema Kayombo.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

1 Comments

  • avatar
    Jusseim Mwakipesile
    30/12/2020

    Kwanini hashauriani na Katibu Mkuu Utumishi ?

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi