loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Barcelona yabanwa bila Messi

BARCELONA wamejikuta katika wakati mgumu wakati wakicheza bila nyota wake majeruhi, Lionel Messi pale walipolazimishwa sare nyumbani dhidi ya timu inayopambana isishuke daraja ya Eibar katika mchezo wa La Liga juzi Jumanne.

Martin Braithwaite alikosa penalti katika kipindi cha kwanza kabla Eibar hawajawaadhibu wenyeji wao kwa bao la kuongoza katika dakika ya 57 kupitia kwa mshambuliaji wao, Kike Garcia.

Wenyeji walipambana na kusawazisha kwa bao la Ousmane Dembele alilofunga dakika 10 baadae, likiwa shuti lake la kwanza golini. Braithwaite alipata nafasi ambayo kama angeitumia vizuri angewawezesha wenyeji kuibuka na ushindi baada ya kuwa katika nafasi nzuri, lakini alipiga shuti lililopaa juu ya lango licha ya kuwa karibu kabisa na goli.

Messi, ambaye anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu, aliushuhudia mchezo huo akiwa jukwaani, baada ya kuwasili kutoka kwao Argentina mapema siku ya mchezo huo.

Pointi hiyo moja inawaacha Barcelona katika nafasi ya sita ya msimamo wa Ligi Kuu hiyo ya Hispania wakati Eibar wenyewe wako katika nafasi ya 14 , pointi mbili juu ya ukanda wa kushuka daraja.

REAL Madrid imekaa kileleni mwa msimamo wa La Liga baada ...

foto
Mwandishi: BARCELONA, Hispania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi