loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ronaldo na wenzake waukaribisha mwaka mpya

NYOTA wa michezo duniani kote wamewatakia watu Heri ya Mwaka Mpya huku wakiuaga mwaka 2020.

 

Kuanzia mwana soka mkubwa Cristiano Ronaldo hadi kwa bingwa wa medali za dhahabu wa Olimpiki na mwanariadha anayeshikilia rekodi Usain Bolt, ambaye ni alama katika michezo duniani wamefurahia kumaliza mwaka na wapendwa wao.

 

Hatahivyo, wengi wao wakisheherekea wakiwa majumbani na wapendwa wao badala ya kuwa nje ya nyumba zao kutokana na mlipuko wa janga la virusi vya corona, ambavyo vimesababisha kuwepo na vikwazo katika sherehe.

 

Mshambuliaji wa Juventus, Ronaldo alionekana katika picha akiwa pamoja na rafiki yake wa kike, Georgina Rodriguez na watoto wao, huku sebule ikiwa imepambwa kwa maputo na mapambo mengine.

 

Kwingineko katika soka, nahodha wa Liverpool Jordan Henderson alionekana akiwa na jioni tulivu wakati akipata chakula kilichopikwa nyumbani kwake pamoja na bia.

 

Kiungo huyo wa England aliandika: 'Mlo wa Mkesha wa Mwaka Mpya…nawatakia heri ya mwaka mpya wote'

 

Kkosi cha kocha Jurgen Klopp, ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya England kilikuwa na siku chache zaidi za mapumziko kabla ya kucheza mchezo wao ujao Jumatatu dhidi ya Southampton.

 

Mshambuliaji wa Atletico Madrid na mchezaji mwenzake wa zamani Henderson hapo Anfield, Luis Suarez alionekana mwenye furaha sana akipozi kwa picha akiwa na familia yake.

 

Suarez aliondoka Barcelona baada ya kuwasili kwa kocha Ronald Koeman katika kipindi cha majira ya joto na kilikuwa chanzo cha kuondoka kwake hapo Nou Camp baada ya kutopewa kipaumbele na kocha huyo.

 

Mchezaji huyo aliandika: 'Mwaka 2020 unaoondoka, ni mwaka mgumu kwa kila mmoja wetu. Mwaka ulifanya watu wote duniani kutaabika kutokana na janga la virusi vya corona, acha tuangalie mbele…Nawatakia kila la heri kwa mwaka huu wa 2021, nawatakia afya njema na HERI YA MWAKA MPYA !!!!

 

Mshambuliaji wa Manchester United, Jesse Lingard alionekana mwenye furaja huku akipiga picha akiwa ameonesha alama ya dole gumba karibu la alama inaonesha mwaka '2021'.

 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alitoa maelezo ya picha: 'Maajabu katika kuuanza mwaka…Heri ya Mwaka Mpya, Muanze mwaka 2021 mkiwa na Afya Njema, Mafanikio na Furaha.'

 

Mchezaji mwenzake wa Man United, Nemanja Matic alitupia picha zake akiwa amevalia mavazi ya `Father Christmas’  pamoja na mwenzake na watoto, ambao pia waliwatakia wafuasi wao furaha ya mwaka mpya.

 

Kiungo wa Everton, James Rodriguez akiwa amevalia shati jeusi pamoja na jinsi akifurahi mbele ya maputo yaliyoandikwa '2021' akiwa pamoja na mtoto wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja, Samuel.

 

Bingwa wa medali za dhahabu za Olimpiki na mtu mwenye kasi zaidi duniani, Usain Bolt alionekana katika picha akiwa na marafiki zake na familia yake wakati wakiukaribisha mwaka mpya, 2021.

 

Nyota huyo wa mbio za uwanjani na rafiki yake wa kike, Kasi Bennett ambao kwa mara ya kwanza walianza urafiki wao hivi karibuni.

 

Kipa wa Manchester City, Ederson alionekana mwenye furaha kubwa akiwa na mke wake, Lais Moraes wakisheherekea mwaka mpya.

KUMEKUWA na zogo kwenye soka la Ulaya tangu ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi