loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Murray ajitoa mashindano ya ATP

MUINGEREZA bingwa namba moja wazamani wa dunia, Andy Murray amejitoa katika mashindano ya wiki ijayo ya ATP yatakayofanyika Delray Beach – lakini sio kwasababu ya kuumia.

 

Murray alikubali kushiriki mashindani hayo ambayo ni mwanzo wa msimu wa mwaka 2021 akianzia hatua ya awali katika mashindayo hayo ya Florida.

 

"Ni wazi kuongezeka kwa kiwango cha Covid-19 na jinsi wanavyopambana nacho, nataka kupunguza hatari kuelekea mashindano ya Australian Open," alisema mchezaji huyo wa Scotland.

 

Wachezaji itabidi kupita vipimo kadhaa vya Covid wakati wa karantini ya siku 14 huko Melbourne kabla ya kuanza kwa mashindano hayo makubwa.

 

Muingereza namba moja Dan Evans naye pia ameamua kutoshiriki mashindano hayo ya Delray Beach, ambako alifungwa katika fainali mwaka 2019.

 

Evans, 30, alisema kuwa hayuko tayari kushindana na badala yake atafanya mazoezi zaidi kwa wiki kadhaa akijiandaa kwa mashindano ya Australian Open.

 

Mashindano hayo yanatarajia kuanza Februari 8 baada ya kusogezwa mbele kwa wiki tatu kutokana na janga la virusi vya corona.

 

Kushiriki kwa Murray katika mashindano hayo ya Melbourne Park kunakuja miaka miwili baada kucheza mashindano hayo na hilo linaokana kama ni mechi yake ya mwisho kama mchezaji wa kulipwa.

 

Akiwa wa 122 kiviwango duniani, Murray alikuwa katika nafasi ya chini sana kuingia moja kwa moja katika mashindano hayo, hivyo mchezaji hyo mwenye umri wa miaka 33, mshindi wa pili mara tano wa Melbourne, alipewa nafasi ya kuanzia chini.

 

Bingwa huyo mara tatu wa mashindano makubwa aliweza kucheza mechi rasmi saba mwaka jana kwa sbabu ya maumivu, na kufungiwa kwa miezi mitano kushiriki mashindano.

 

Murray alionekana yuko vizuri Desemba katika mashindano ya maonesho ya Waingereza, baada ya kumchapa Muingereza namba moja Dan Evans na yule anayeshikilia nafasi ya tatu, Cameron Norrie kwa seti mfululizo.

 

KUMEKUWA na zogo kwenye soka la Ulaya tangu ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi