loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Man City an City pungufu yaifuata Chelsea

TIMU ya Manchester City inaifuata Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England bila ya wachezaji wake watano baada ya kukumbwa na virusi vya corona, imeelezwa.

Kyle Walker, Gabriel Jesus na wachezaji wengine watatu, ambao hawajatajwa kwa sasa wamejitenga kwa utaratibu wa ugonjwa huo. “Sifikiri kama Ligi Kuu inaturuhusu kuwatangaza wachezaji hao, lakini mtajua (Jumapili), “ alisema Guardiola.

Mchezo wa Man City uliopangwa kufanyika Desemba 28 uliahirishwa baada ya baadhi ya wachezaji kupimwa na kukutwa na virusi vya corona, lakini wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza walipopimwa hawakukutwa na corona.

Guardiola alisema pamoja na kuwakosa wachezaji hao watano, lakini Man City bado ina kikosi kipana, ambacho kingeweza kucheza katika mchezo huo wa Goodison Park lakini mchezo uliahirishwa kwa sababu majibu ya vipimo yaliletwa mapema siku hiyo hiyo.

“Tulitaka kucheza lakini siku ya mchezo, kulikuwa na kesi kibao, tuliijulisha Bodi ya Ligi Kuu, “alisema Guardiola.

“Binafsi nilimuita (kocha wa Everton) Carlo Ancelotti kumuelezea hali ilivyo kwa sababu siku moja kabla ya mchezo ule tuliwasiliana kuhusu nini kitatokea na hatari kubwa iliyopo.”

Winga wa Chelsea Hakim Ziyech atacheza kwa mara ya kwanza tangu apate maumivu mapema Desemba timu yake ilipokuwa ikicheza dhidi ya Leeds kwenye Uwanja wa Stamford Bridge. Beki Reece James ataukosa mchezo huo kwa tatizo kama hilo.

Chelsea imepoteza mechi zake tatu za ugenini katika ligi, lakini kiwango chao wanapokuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Stamford Bridge kimewafanya kuwa imara zaidi.

ZILIPOKUTANA

Manchester City imepoteza mechi 26 za Ligi Kuu ilipokutana na Chelsea, ikiwa ni zaidi ya timu nyingine yeyote. City inaweza kupoteza mechi ya tatu mfululizo ya ugenini dhidi ya Chelsea kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2006 hadi 2009.

CHELSEA

Chelsea imeshinda mechi moja kati ya tano za Ligi Kuu, ikipata pointi nne kutoka katika 15 zilizotakiwa. Hatahivyo, kufungwa mara 14 katika mechi za ligi za nyumbani kulitokea walipocheza dhidi ya Liverpool Septemba (wakishinda 10, kutoka sare tatu).

The Blues haijashinda mechi zake za ufunguzi za Ligi Kuu katika misimu minne iliyopita. Bao lao pekee katika mechi nne dhidi ya wapinzani wake waliopo katika nafasi ya sita bora msimu huu, lilifungwa na Tammy Abraham wakati Chelsea ilipofungwa 3-1 dhidi ya Arsenal Boxing Day.

Olivier Giroud alifunga mara 11 katika mechi 14 alizoanza za Ligi Kuu mwaka 2020. Timo Werner amecheza mechi 11 bila ya kufunga bao lolote kwa Chelsea.

MAN CITY

Manchester City haijafungwa katika mechi 10 katika mashindano yote, ikishinda mara saba na kutoka sare mara tatu. Pointi 26 ilizonazo sasa, bado ni idadi ndogo kwake baada ya kushuka dimbani mara 14 katika kipindi cha miaka 10.

Man City inaweza kushinda mechi tatu mfululizo katika ligi kwa mara ya kwanza msimu huu. Walipoteza mechi tatu zilizopita za Ligi Kuu jijini London, wakitoka sare nyingine.

Man City haijafungwa katika mechi 13 za mashindano yote msimu huu, ikiwa ni zaidi ya timu nyingine yeyote katika tano bora ya ligi za Ulaya. Sergio Aguero alifunga mabao 10 katika mechi zake tisa za mwisho dhidi ya Chelsea. Hatahivyo, kwa sasa hajafunga katika mechi 10 za Ligi Kuu inayoendelea.

KUMEKUWA na zogo kwenye soka la Ulaya tangu ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi