loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Juventus katika mtihani Serie A ikiendelea

KATIKA kipindi cha karibu muongo mmoja, Serie A imekuwa nyepesi kwa Juventus lakini timu hiyo yenye maskani yake Turin inapambana kupanda mlima ili kufanya vizuri msimu huu.

Juventus ambao ndio mabingwa watetezi wa Serie A, kwa sasa wako katika nafasi ya sita baada ya kujikusanyia pointi 24 huku AC Milan na Inter Milan zikiwa katika nafasi ya kwanza na pili zikiwa na pointi 34 na 33.

Juve leo Jumapili itaikaribisha Udinese wakati Serie A ikiendelea baada ya kusimama kwa siku 10 ikiwa ni mapumziko ya Krismas na Mwaka Mpya, 2021, ambayo imewapa muda mzuri wa maandalizi baada ya kufungwa 3-0 dhidi ya Fiorentina.

Mchezaji anayeongoza kwa kupachika mabao, Cristiano Ronaldo alitumia kipindi hicho akiwa Dubai, ambako alikuwa akila maisha na familia yake.

Katika msimu wa kwanza chini ya Andrea Pirlo, mtu ambaye huko nyuma hakuwa na uzoefu wa kufundisha soka, Juventus imejikuta katika nafasi ya sita ikiwa na pointi zake 24, 10 nyuma ya vinara AC Milan, lakini bado wana mchezo mmoja mkononi.

KUMEKUWA na zogo kwenye soka la Ulaya tangu ...

foto
Mwandishi: TURIN, Italia

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi