loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Arteta kusubiri rteta kusubiri hatma ya Ozil

KLABU ya Arsenal itatathmini hatma ya mchezeshaji Mjerumani Mesut Ozil mwishoni mwa kipindi cha dirisha dogo la uhamisho la Januari, alisema kocha Mikel Arteta.

Ozil hajaichezea Arsenal tangu Machi na hakuwemo katika orodha ya kikosi hicho katika nusu ya kwanza ya msimu wa Ligi Kuu ya England na michuano ya Ligi ya Ulaya.

Mjerumani huyo ambaye ni mmoja wa wachezaji wanaolipwa zaidi katika kabu hiyo, atamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu.

Lakini Arsenal inaangalia uwezekano wa kupunguza baadhi ya wachezaji katika dirisha hili la usajili mwezi huu ili kupunguza kikosi chake, kuongeza uwezekano wa kurejeshwa tena kwa Ozil katika kipindi cha pili cha msimu.

Wakati alipoulizwa kuhusu kurejea kwa mchezaji huyo nyota mwenye umri wa miaka 32, Arteta aliwaambia waandishi wa habari: “Tutaangalia nini kitatokea katika kipindi cha dirisha la usajili na tutatathmini mwishoni.”

Arteta pia alisema kuwa klabu haiangalii kukata mikataba ya wachezaji ambao hawako katika mpango wake.

“Unatakiwa kuheshimu mikataba ya wachezaji, “aliongeza. “Unachotakiwa kufanya ni kuwa wazi kwao, waeleze nia yako, jukumu walilonalo katika timu na kwanini hilo liko hivyo.”

Arsenal, ambao kimsimamo kwa sasa wako katika nafasi ya 13 katika Ligi Kuu wakiwa na pointi 20, jana walitarajia kucheza dhidi ya West Bromwich Albion.

KUMEKUWA na zogo kwenye soka la Ulaya tangu ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi