loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mauricio Pochettino Sababu za kujinga na Paris St-Germain

IKIWA miezi 13 tangu alipooneshwa mlango wa kutokea katika klabu ya Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino amerejea tena katika soka la kiwango cha juu baada ya kutua kwa matajiri wa Ufaransa wa Paris St-Germain. (PSG).

Baada ya tetesi za muda mrefu, PSG juzi ilimtangaza rasmi kocha huyo wa wazamani wa Tottenham na Southampton Pochettino (48) kuwa kocha wao mkuu akichukua nafasi ya  Thomas Tuchel na ataifundisha timu hiyo hadi Juni 30, 2022.

Pochettino, ambaye aliichezea PSG kati ya mwaka 2001 na 2003, alikuwa hana kazi tangu alipotimuliwa na uongozi wa Spurs Novemba mwaka 2019.

Kimsimamo wa Ligue 1, PSG wako katika nafasi ya tatu na Februaria na Machi watakutana na vigogo Barcelona katika mechi za michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya katika hatua ya 16 bora,

Kocha Mjerumani Tuchel alitimuliwa Desemba 29, 2020 baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka miwili na nusu.

SABABU KUBWA

Pochettino amerudi katika soka, lakini swali kubwa ni kwanini kocha huyo ametua PSG?

Pochettino jana Jumapili alitarajia kuanza kazi rasmi ya kuifundisha timu hiyo wakati ikinza mazoezi kufuatia mapumziko ya kipindi cha majira ya baridi.

Alisema ni mtu mwenye furaja kubwa na heshima kubwa kuchukua majukumu hayo katika klabu huyo, hasa ukizingatia wakati wote ilikuwa katika nafasi maalum katika moyo wake.

"Leo nimerudi katika klabu na ni furaha kubwa kufanyakazi na wachezaji wakubwa na wenye vipaji vya hali ya juu, “alisema Pochettino.

"Timu hii ni ya ajabu na iliyojaa vipaji na mimi na wafanyakazi wenzangu tutafanya kazi kwa bidii hapa Paris St-Germain katika mashindano yote. Pia tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha timu yetu inakuwa na alama ya kushambulia itakayowafurahisha mashabiki."

Mwenyekiti wa PSG na Mtendaji Mkuu, Nasser Al-Khelaifi alisema kurejea kwa Pochettino ni jambo zuri na kubwa katika klabu yao, ambayo ina malengo kibao ya kufanya vizuri.

Wakati akiwa nje ya kazi ya ukocha, Muargentina huyo alijaribu kufanya mazungumzo na klabu kibao, zikiwemo Benfica na Monaco, na pia aliwahikufuatwa na Barcelona na Real Madrid, ingawa hakuna ofa rasmi iliyotolewa.

Lakini sasa mambo yamekamilika kwa Pochettino na kuwa kocha wa klabu hiyo yenye maskani yake katika Uwanja wa Parc de Princes.

Akiwa kama mchezaji wazamani wa klabu hiyo ambaye alifurahia misimu yake miwili na nusu hapo PSG, uamuzi wake wa kukubali kibarua hicho litakuwa ni jambo zuri, kwani ametua katika timu anayoijua.

Tuchel tayari alikuwa ameshauambia uongozi wa PSG kuwa hana mpango wa kuendelea nao katika msimu ujao.

Tuchel ni mmoja wa makocha wa kisasa wa Ujerumani, ambao wanaujua vizuri mchezo wa soka, hasa kucheza pamoja tofautia na kutoa kipambele kwa mchezaji mmoja mmoja.

Anajua kuwa katika klabu kama PSG kuna umuhimu wa nyota mmoja mmoja kama akina Kylian Mbappe na Neymar kwa wachezaji kama hao huwa na mawasiliamo ya moja kwa moja na Rais wa klabu.

Licha ya kuwa mshindi wa pili katika michuano ya Ligi ya Mabingwa, ameacha klabu hiyo ikiwa mabingwa wa Ufaransa  katika misimu saba kati ya nane iliyopita, na hivi sasa wako katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligue 1.

PSG wako pointi mkoja tu nyuma ya vinara Lyon na Lille wanaoshika nafasi ya kwanza na pili kila moja ikiwa na pointi 35, pamoja na kuwa na nafasi ya kutetea taji lao, lakini hizi ndizo pointi chache zaidi kwa timu hiyo kuwahi kuwa nazo katika hatua hii tangu msimu wa mwaka 2013-14.

Pointi 14 kutoka katika mechi 24 zinaweza kutosha kwa timu yoyote, lakini Tuchel anaondoka PSG ikiwa imepoteza mechi nne kati ya 17 za kwanza.

Msimu uliopita, kabka ligi haijafutwa baada ya mechi 27,walikuwa wamepoteza mechi tatu tu. Lakini kutimuliwa kwa kocha huyo kulikuwa na ulazima ili kuiwezesha timu hiyo kufanya vizuri zaidi.

Mtazamo mkubwa wa klabu hiyo msimu uliopita ulikuwa ni wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kufuatia maelekezo aliyopewa katika barua.

Wakati wa kampeni hiyo timu illionesha umoja hasa baada ya chakula cha usiku katika mgahawa wa Marco Verratt,  ambako waliahidi kufanyakazi kama timu, ambapo walitoka nyuma kwa kufungwa 2-1 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Borussia Dortmund na kushinda mchezo wa marudiano kwa mabao 2-0 nyumbani na kutinga robo fainali kabla ya kuibuka kwa corona.

Lakini msimu huu imedhihirisha kuwa haiwezekani kuibua ari hiyo, huku kocha Tuchel akiwa haelewani na mkurugenzi wa soka Leonardo.

Kocha huyo alikuwa Qatar kufuatia mualiko kutoka kwa Kamati ya Kombe la Dunia, huku wachezaji kibao wamemuona kama mtu mwenye busara kubwa.

Pochettino hana wakala, hakuna mtu aliyepanga mawasiliano  ya moja kwa moja na kocha huyo mambo yake hufanya mwenyewe moja kwa moja.

Pochettino sasa ana jukumu la kufanya kazi na wachezaji tofauti tofauti, huku akilijua vizuri hilo.

Ukiwa katika klabu kama PSG na ile ya Real Madrid, wenyewe mamabo yao wanayaendesha tofauti kabisa na klabu kama Southampton na Spurs.

KUMEKUWA na zogo kwenye soka la Ulaya tangu ...

foto
Mwandishi: PARIS, Ufaransa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi