loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ronaldo apiga mbili Juve ikishinda 4-1

NYOTA Cristiano Ronaldo alifunga mara mbili na kutengeneza bao jingine wakati Juventus ikiibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Udinese katika mchezo wa ligi ya Serie A.

Ronaldo alifunga bao la kwanza katika dakika ya 31, baada ya pasi ya Aaron Ramsey huku akifunga jingine katika dakika ya 70.

Kwa mabao hao ya juzi, Ronaldo amefikisha mabao 14 kutoka katika mechi 11 za ligi.

Mabao mengine ya Juventus yaliwekwa kimiani na Chiesa katika dakika ya 49, huku lile la nne likifungwa na Paulo Dybala katika dakika za majeruhi wakati bao la kufutia machozi la wapinzani wao likifungwa na Marvin Zeegelaar katika dakika ya 90.

Kikosi hicho kinachofundishwa na kocha Andrea Pirlo sasa kipo pointi 10 nyuma ya vinara AC Milan, ikiwa na mchezo mkononi, wakati Udinese imeporomoka hadi katika nafasi ya 13 na haijashinda mchezo wowote hadi sasa.

KUMEKUWA na zogo kwenye soka la Ulaya tangu ...

foto
Mwandishi: TURIN, Italia

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi