loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wenye sifa ndio wawanie uongozi Riadha Tanzania

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) umepangwa kufanyika Januari 30 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jiini Dar es Salaam ili kupata viongozi watakaoongoza mchezo huo kwa miaka minne ijayo.

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) juzi lilitangaza tarehe na utaratibu mzima wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu ili kupata wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi.

Utoaji na urejeshaji fomu utahitimishwa Januati 19 kabla ya mchujo kufanyika Januari 21 ili kupata wagombea rasmi, ambao watapigiwa kura na wapiga kura katika nafasi mbalimbali zinazogombea.

Nafasi zitakazoshindaniwa baada ya kufanyika kwa marekebisho ya Katiba ni pamoja na Rais na Makamu wake, ambao kila mgombea atalipa kiasi cha Sh 200,000 kwa fomu wakati wajumbe watatoa Sh 100,000 kwa kila mgombea.

Katika mabadiliko hayo ya Katiba, RT sasa itakuwa na makamu mmoja wa rais badala ya wawili, huku katibu mkuu na mhazini kuanzia sasa watakuwa waajiriwa na sio kuchaguliwa tena.

Baada ya kutangazwa kwa utaratibu huo sasa ni wakati wa wadau wa michezo wenye sifa stahiki kujitokeza kwa wingi, hasa katika utaratibu wa sasa, ambao wajumbe wa Kamati ya Utendaji watapatikana kikanda.

 Wapo wadau wengi wa michezo wenye sifa katika nyanja mbalimbali, lakini wale wenye sifa wamekuwa wagumu kujitokeza na badala yake ndio wamekuwa mstari wa mbele kulaumu mambo yanapoharibika.

Ni matarajio yetu watu wenye sifa na taaluma zao katika michezo watakuwa mstari wa mbele kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili kuurejesha mchezo huo kileleni kama ilivyokuwa zamani.

Watanzania tumechoka kuwa wasindikizaji katika riadha na hata michezo mingine, kwani huko nyuma Tanzania ilifanya maajabu katika mchezo huo kiasi cha   kutisha duniani, lakini sasa hatutambuliki tena katika mchezo huo kuanzia Afrika Mashariki, Afrika na duniani kwa ujumla.

Wapiga kura ambao ni viongozi wa  vyama vya mikoa ndio wenye jukumu la kuchagua viongozi, hivyo wanatakiwa kuwa makini sana ili kuhakikisha wanachagua viongozi wenye uwezo wa kuleta mafanikio katika mchezo huo na kuondoa ubabaishaji.

 Kikubwa ni kuacha au kuondoa ubinafsi kwa wapigaji kura, hivyo wanatakiwa kufikiria maendeleo ya mchezo badala ya kila mmoja kujifikiria yeye na atafaidikaje na mchezo huo.

 

BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) juzi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi