loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba sajilini kujiimarisha zaidi

KWANZA naipongeza Simba kwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini nawakumbusha kuwa safari ndio imeanza, hivyo wanatakiwa kufanya usajili katika safu ya ulinzi na kiungo ili kuimarisha kikosi.

Simba kuingia hatua ya makundi msimu huu, tayari Tanzania imeingia katika ligi 12 bora za Afrika, ambazo hupewa nafasi nne za uwakilishi kwenye mashindano ya Afrika, mbili Ligi ya Mabingwa na mbili Kombe la Shirikisho.

Kwa maana hiyo mashindano ya Afrika msimu wa 2021/22, Tanzania itatoa timu nne kama ilivyokuwa msimu wa mwaka 2019/20.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Simba inaruhusiwa kusajili mchezaji mmoja hadi saba kwa ajili ya kujiimarisha na mechi za hatua ya makundi.

Hivyo ili Simba ifanye vizuri kama ilivyofanya msimu wa 2018/2019 wanatakiwa kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi, ambao watakuja kushirikiana na wachezaji waliopo.

Mabeki waliopo Simba ni wazuri lakini wana umri mkubwa, hivyo wakikutana na washambuliaji vijana kama Luis  Miquissone kuhimili kasi yao itakuwa ni ngumu japo watu wanasema uzee dawa lakini si kila wakati.

Katika safu ya kiungo pia inahitaji kuongezewa nguvu kwani wachezaji waliopo hawatoshi kuipeleka Simba robo fainali japo hivi karibuni walimsajili Thadeo Lwanga.

Msimu wa 2018/2019 wakati Simba inafundishwa na Patrick Aussems ilikuwa na kikosi bora zaidi na wachezaji walikuwa katika kiwango kizuri pia kikosi cha Sven Vandenbroeck aliyetimuliwa juzi nacho si kibaya, kwani kinacheza kwa mbinu na kitimu zaidi.

Kipindi kile Meddie Kagere, Jonas Mkude, na Erasto Nyoni na Emanuel Okwi walikuwa wazuri sana na sasa wana uzoefu, lakini sasa kuna Clatous Chama na Luis Miquissone ambao hawakamatiki kutokana na uwezo walionao.

Katika droo iliyotarajiwa kuchezeshwa jana Cairo nchini Misri, Simba huenda ikakutana na timu ambazo ilicheza nazo msimu wa 2018/2019, ambazo nazo zimefuzu tena hatua ya makundi.

Msimu wa 2018/19 katika makundi Simba ilikutana na AS Vita, Al Ahly na JS Saoura ambayo haijafuzu msimu huu, lakini katika hatua ya robo fainali ilikutana na TP Mazembe na ikaondolewa kwa jumla ya mabao 4-1.

AS Vita, Al Ahly na TP Mazembe zimefuzu makundi na Simba inaweza kukutana na aidha timu mbili kati ya hizi au zote, na hii inaweza kuwa faida kwao kwa sababu wanajuana.

Kwa mtazamo wangu,  Simba inahitaji kujiimarisha kila idara maana utakumbuka kuwa katika michezo ya ugenini ilikuwa ikifungwa na ikija kucheza nyumbani inapata matokeo mazuri.

Hatutegemei Simba ikiishia hatua ya robo fainali bali itafika nusu na hata fainali maana soka la sasa siyo historia bali jinsi utakavyochanga karata zako na kusajili wachezaji wenye viwango utapata matokeo mazuri.

BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) juzi ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi