loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uturuki, Ufaransa mbioni kurejesha uhusiano Uturuki

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu amesema nchi yake na Ufaransa zinafanya jitihada ya kurejesha uhusiano na kueleza kuwa mazungumzo kati yao yanaendelea vizuri.

Cavusoglu alisema kuwa Uturuki iko tayari kuboresha uhusiano na mshirika wake wa NATO, Ufaransa ambayo pia imeonesha nia hiyo.

Uturuki na Ufaransa zimekuwa katika malumbano kuhusu sera za Syria, Libya, mashariki mwa Mediterania na Nagorno-Karabakh. Pia zinavutana kuhusu kuchapishwa kwa katuni za Mtume Muhammad (S.A.W) nchini Ufaransa.

Ufaransa kwa upande wake imekuwa ikiongoza shinikizo la vikwazo vya Umoja wa Ulaya (EU) dhidi ya Uturuki.

Baada ya mvutano wa miezi kadhaa sasa, Rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron walizungumza kuhusu tofauti zao kwa njia ya simu Septemba mwaka jana. Katika mazungumzo hayo walikubaliana kuboresha uhusiano kati ya nchi zao.

WANACHAMA wa Chama cha Republican nchini ...

foto
Mwandishi: ANKARA, Uturuki

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi