loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tuwezeshe wananchi kutumia soko la China

JANA Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amewataka watanzania kujipanga kutumia soko la China kuweza kuleta mabadiliko katika maisha yao kwa kuongeza kipato.

Aidha alisema wazi kwa Watanzania kwamba wasiwe na shaka na fursa hiyo kwa kuwa China imeahidi kuendelea kuwa bega kwa bega na nchi za Afrika na Tanzania ikiwamo.

Pamoja na kumpongeza Waziri Kabudi kwa kauli hiyo njema kwa watanzania tunapenda kuwakumbusha watuw anaohusika na masoko kuanza kujipanga kimkakati na kusaidia  watu kutumia fursa hiyo vyema.

Wakulima wetu na wafanyabiashara wadogo ambao ndio msingi mkubwa wa uzalishaji nchini hawajui mambo mengi yanayohusu biashara za kimataifa hivyo kiukweli ipo haja kwa maofisa wa serikali kuachana na  ofisi zao na kwenda kuwaona wadau hawa moja kwa moja ili  tuingie soko la China kwa miguu yote miwili.

Tunasema hivyo tukijua kwamba ni nadra sana kwa watanzania kupata nafasi na kuzitumia kwa kuwa hawajui nini wanachostahili kuifanya na kwa mipangilio gani.

Tatizo letu hili ni la muda mrefu na ndio ambalo limefanyika hata katika kutoa walimu wa Kiswahili tukishindwa kutumia nafasi zilizopo na majirani zetu kutwaa nafasi hizo.

Kwa kuelewa tatizo hili tunahofu kwamba maagizo ya Profesa Kabudi ya kutumia fursa ya soko la China huenda nayo ikatupita kama Kiswahili kinavyotupita  kama maofisa wetu kuanzia wale wa uzalishaji iwe kwenye kilimo au viwandani, ubora wa bidhaa hawatatoka na kwenda kuwa bega kwa bega na wanaotaka kupenya soko la China.

Tunaamini kwamba kama wataalamu wetu watakuwa bega kwa bega na wafanyabiashara wawe wadogo , wa kati au wakubwa watanzania tuna mambo mengi ya kupeleka soko la China .

Kwa kuwa moja ya makubaliano katika mazungumzi ya nchi hizo mbili ni wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Baraza la Taifa la China, Wang Yi ni Tanzania kufanya biashara na kuuza zaidi nchini China, wakati umefika wa kutumia urafiki wetu kuneemesha Watanzania.

Kwa kuwa mahusiano ya Tanzania na China ni ya kipekee, watanzania wanatakiwa kutumia kila fursa iliyopo kufuangua biashara zaidi, Tanzania kuuza zaidi bidhaa zake nchini China, iwe mazao ya kilimo yaliyoongezwa thamani au  mazao ya uvuvi ama mifugo

Watanzania tunapaswa kutambua kwamba China ina wananchi bilioni 1.5, ni soko kubwa sana tunachotakiwa ni kujipanga kujua wanahitaji nini  ili na sisi tupeleke bidhaa hizo.

Tunawaomba  watanzania kwa ujumla wao kuamka na kuwasukuma wataalamu wetu kwa kutambua kwamba kazi kubwa ambayo sisi inastahili kufanywa ni kwa wananchi kujenga uwezo wa pamoja wa kufanikisha utimizaji wa matakwa ya soko iwe kwenye kilimo madini au viwandani kwa lengo la kunufaika nalo.

BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) juzi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi