Ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la Sriwijaya kutoka nchini Indonesia iliyobeba abiria zaidi ya 60 na kutojulikana ilipo, imekutwa imeanguka baharini katika Mji Mkuu wa nchi hiyo Jarkata.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na vikosi vya uokoaji vya nchi hiyo imeeleza kukutwa kwa baadhi ya sehemu za miili ya binadamu, koti za kuokoa maisha na mabaki wa ndege hiyo.
Ndege hiyo ya Boeing 737-500 ilikuwa imebeba watu 62, wakiwemo abiria 56 na wafanyikazi sita.