loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ni Simba, Yanga, Namungo Mapinduzi

TIMU za Soka za Simba, Namungo  na Yanga  zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani hapa.

 

Namungo imefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kupata nafasi ya best Looser wakati Simba na Yanga walifikia hatua hiyo baada ya kushinda nafasi za kwanza katika makundi yao.

 

Simba ambayo ilikuwa katika Kundi B imeshika nafasi ya kwanza baada ya kushinda michezo yote miwili na kuwa na pointi sita kundi ambalo lilikuwa na bingwa mtetezi Mtibwa Sugar ambayo imeutema ubingwa huo baada ya kufungwa mabao 2-0 na Wekundu wa Msimbazi.

 

Hivyo Simba kwa matokeo hayo leo itacheza na Namungo katika mchezo wao utakaoanza saa 2:00 usiku katika Uwanja wa Amaan, ambao ndio unaotumika kwa michuano hiyo.

 

Kwa upande wa timu ya Yanga, nao watashuka dimbani mapema leo kuanzia majira ya saa 10:00 jioni akicheza ama na Azam na Malindi atakayeshinda mchezo wao wa jana usiku.

 

 Yanga imetinga nusu fainali baada ya kujikusayia pointi nne baada ya kushinda mchezo mmoja na kutoa sare mmoja.

 

Mchezo wa Simba na Namungo unatarajia kuwa mkali na wa kusisimua baada ya timu zote hizo kutoka katika michuano ya kimataifa, Simba lIgi y Mabigwa na Namungo Shirikisho Afrika.

 

Wakati huohuo, kiwango cha mshambuliaji wa timu ya Simba, Miraji Athuman katika michuano ya Kombe la Mapinfuzi kimeonesha kumvutia kocha Seleman Matola.

KOCHA Mkuu wa Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi