loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kocha mpya Gor mtegoni

KOCHA Mkuu mpya wa Gor Mahia Carlos Manuel Vaz Pinto amekabidhiwa majukumu mazito ili kurejesha hadhi ya klabu hiyo katika kiwango cha bara kwa kuiongoza kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Pinto, kwa mujibu wa makamu wa mwenyejiti wa klabu hiyo, Francis Wasuna, mwenye leseni ya ukocha ya Uefa, aliingia mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha timu hiyo, akichukua mikoba ya Mbrazil Roberto Oliveira aliyeondoka katika klabu hiyo Desemba baada ya kushindwa kukidhi vigezo vya Caf.

 

Mabingwa hao wa Kenya walimuazima kocha wa Posta Sammy "Pamzo' Omollo aliyewasaidia wakati wa raundi ya awali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika wakati kocha msaidizi wazamani Patrick Odhiambo alikuwa akiisimamia timu hiyo katika mechi za ligi.

 

Gor ilitolewa kwa aibu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika baada ya kufungwa kwa jumla ya mabao 8-1 katika raundi ya kwanza dhidi ya mabingwa wa Algeria, CR Belouizdad katika raundi ya kwanza wiki iliyopita.

 

Kipigo hicho kizito kilishuhudia timu hiyo ikitolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika na kuangukia katika Kombe la Shirikisho na sasa itakutana na timu ya Zambia ya Napsa Stars katika mchezo wa mchujo na mshindi atatinga hatua ya makundi.

 

Gor Mahia inatarajia kuikaribisha Napsa Stars katika mchezo wa kwanza wa mchujo utakaofanyika Februari 14 kabla ya kurudiana ugenini wiki moja baadae.

 

Wasuna alibainisha kuwa kocha huyo Mreno, ambaye ameingia mkataba wa miaka miwili, anatakiwa kuifungisha virago Napsa katika mchezo wa mchujo na kuirudisha klabu hiyo katika hatua ya makundi.

 

Kógalo kwa mara ya mwisho ilicheza hatua ya makundi mwaka 2019 ikiwa chini ya kocha Hassan Oktay, ambako walipangwa Kundi 'D' na kutinga hatua ya robo fainali.

 

"Tunamtaka kuipeleka klabu katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, pamoja na kushinda ligi na tumempa muda wa kutosha ili kufikia malengo hayo, " alisema.

KOCHA Mkuu wa Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi