loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ummy awaonya wataalamu elekezi wasio waaminifu

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Ummy Mwalimu ametoa onyo kwa wataalamu elekezi wasio waaminifu kwa wawekezaji na wafanyabiashara kwani wamekuwa wakirudisha nyuma juhudi za serikali za kuvutia uwekezaji nchini.

Alitoa onyo hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari akiwa ameambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Geoffrey Mwambe na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Samuel Gwamaka baada ya kutembelea na kukagua mazingira ya kiwanda cha BTY kinachochakata taka hatarishi zinazotokana na betri kilichopo Buguruni jijini Dar es Salaam jana.

Uzalishaji wa kiwanda hicho  ulisimamishwa kutokana na kutokidhi taratibu za mazingira.

Ummy alisema mwekezaji huyo amekwamishwa na mtaalamu elekezi kwa kushindwa kuwasilisha tathmini ya athari kwa mazingira (EIA) kabla ya mradi kuanza.

“Nitafuta vibali vya wataalamu elekezi wote wasiofuata taratibu za kazi zao pamoja na kusiokuwa waaminifu kwani kufanya hivyo kunarudisha nyuma juhudi za serikali katika kufikia uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025,” alisema.

Alisema serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini kwa lengo la kuhamasisha uwekezaji kwa wazawa na wageni kutoka nje ya nchi hivyo ni muhimu kuhakikisha jitihada hizo hazikwamishwi ili kufikia malengo hayo.

Ummy aliitaka NEMC kukutana na uongozi wa kiwanda cha BTY na kuwapa mwongozo utakaokifanya kiwanda kuendelea na uzalishaji sambamba na utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

Alizitaka taasisi zote zinazohusika moja kwa moja na uwekezaji kuacha kufanyakazi za polisi, badala yake zifanye kazi kama washauri hali ambayo itaongeza kasi ya uwekezaji.

“Nitumie nafasi hii kuziasa taasisi zote zinazohusika na uwekezaji kufanya kazi za kiushuri zaidi badala ya kufungia viwanda pindi vinapokiuka kanuni, sheria na taratibu za nchi kwani kufanya hivyo kunapoteza mapato yanayotokana na kodi pamoja na ajira kwa vijana wetu,” alisema.

Kwa upande wake, Mwambe alisema uwapo wa shughuli nyingi kunaongeza wigo wa walipakodi hali ambayo huimarisha uchumi wa nchi.

Naye Dk Gwamaka amewashauri wawekezaji kutafuta wataalamu elekezi wenye weledi na waadilifu na hata wanapokutana na changamoto ya kuwapata wafike ofisi za NEMC makao makuu au ofisi za kanda kwa ushauri zaidi.

“Mawaziri wametutaka ndani ya siku mbili kukutana na mwekezaji kwa ajili ya kutoa maoni yetu ya kitaalamu na tutafanya hivyo kupitia timu ya wataalamu iliyopo,” alisema Dk Gwamaka.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi