loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanzania kutumia kadi kutangaza utalii China

BODI ya Utalii Tanzania (TTB), ubalozi wa China nchini na Kituo cha Utamaduni cha Watu wa China Tanzania wamesaini kadi zitakazokabidhiwa kwa kampuni 17 kuutangaza utalii wa Tanzania kwenye soko la China.

Mwenyekiti wa TTB, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo, Mshauri wa Utamaduni wa Ubalozi wa China na Mkurugenzi wa Utamaduni wa Kituo cha Utamaduni cha Watu wa China nchini, Wang Siping walisaini kadi hizo kwenye ofisi za TTB jijini Dar es Salaam juzi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya utiaji saini hizo, Jaji Mihayo alisema baada ya kusainiwa zitarejeshwa China na kukabidhiwa kwenye kampuni za utalii na kwamba kampuni hizo zitazidurufu na kisha kuzisambaza kwa wateja wao 4,000.

Alisema kadi hizo zitawafikia wateja wao kabla ya Februali 11 ambao ni mwaka mpya wa taifa la China, huku akibainisha kuwa utaratibu wa matumizi ya kadi hizo unaashiria upendo mkubwa wa Watanzania kwa Wachina.

Alisema utaratibu wa matumizi ya kadi hizo ulizinduliwa rasmi Desemba 21 mwaka jana na Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki akishirikiana na kampuni 17 za kusafirisha watalii wa ngazi za juu kutoka soko la nchi hiyo.

Jaji Mihayo alisema kusainiwa kwa kadi hizo ni mwendelezo wa hatua za awali zilizofanywa na Balozi Kairuki na kwamba tayari zimeshaanza kuonesha matunda.

Alitoa mfano kuwa, kampuni ya Fashion Tourism iliandaa timu ya kuzipandisha kadi hizo mpaka kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro na tukio hilo lilitangazwa kwenye vyombo vya habari nchini China.

“Hii ni ishara kubwa ya upendo na kujali watu na kwa kuwa inafahamika mwaka jana Wachina kama raia wengine wa mataifa mbalimbali hawakusafiri nje ya nchi kwa mwaka mzima kutokana na ugonjwa wa homa ya mapafu Covid-19 Tanzania kwa kutumia kadi hiyo inawaalika kuja hapa nchini.

” “Kwa hatua yao ya kuzipandisha hadi katika kilele cha Mlima Kilimanjaro ni ishara ya kuwa mwaka huu wa 2021 utakuwa wenye baraka kwao na tunawakaribisha kuja hapa nchini kutembelea vivutio vya utalii,” alisema. Siping alionesha kuridhishwa na namna TTB inavyotoa ushirikiano kwa kampuni za China zinazotoa huduma za watalii nchini.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi