loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yaanza maandalizi mradi wa umeme Mto Ruhiji

Serikali imesema inatarajia kuanza maandalizi ya ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme katika maporomoko ya Mto Ruhiji kijiji cha Itipula mkoani Njombe utakaozalisha megawati 358, huku timu ya watalaamu wa Serikali ikifika katika maporomoko ya mto huo jana na kufanya ukaguzi. 

Akizungumza mbele ya timu ya watalaamu kutoka Wizara ya Nishati, Tanesco na wakazi wa vijiji vinavyozunguka eneo la mradi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja amesema katika kutekeleza mradi huo, yataanza maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na umeme katika eneo litakalojengwa mabwawa mawili na ‘Intake’.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme (TANESCO) Dk Tito Mwinuka amesema mradi huo ukikamilika utaongeza kiasi cha umeme kwenye Gridi ya Taifa. Mradi huo ambao utajengwa katika kipindi cha miezi 36 unatarajiwa kuanza mwezi Juni mwaka huu.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Isdory Kitunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi