loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Vijana washawishiwa kutumia fursa kujiajiri

VIJANA Jijini Dodoma wametakiwa kujiajiri na kuacha visingizio vya ukosefu wa ajira kwanï fursa zilizopo ni nyingi.

Akizungumza na HabariLEO mmoja wa vijana waliojiajiri katika biashara ya matunda, Hussein Shauri aliwataka vïjana kujiajiri na kuacha visingizio vya ukosefu wa ajira.

Alisema kutokana na uhaba wa ajira yeye kama kijana ameamua kujikita zaidi katika uuzaji wa matunda kwani ni moja ya fursa ambayo ameitumia hasa katika kipindi hiki cha mvua kwani matunda hayo huuzika kwa wingi zaidi.

''Kwenye kipindi kama hiki hasa katika msimu wa mvua huwa tunajichanganya kwenye baadhi ya biashara tofauti tofauti kama sasa hivi tuko na haya matunda ambayo tunayauza, lakini kama kuna kijana ambaye anataka kufanya biashara kama hii mimi niko tayari kumsaidia aje tu hapa tutafanya kazi, hii biashara mimi imenisaidia sana na imenipa faida kubwa na nimepata fedha na kulima mashamba yangu,"alisema.

Alisema kuna vijana watano wanaoshirikiana naye katika uuzaji wa matunda hayo ambayo huyasambaza katika maeneo mbalimbali huku akisema kuwa zipo faida anazozipata kupitia biashara  hiyo.

''Faida inapatikana kiasi fulani sio kukaa hivi hivi, kwa hili tenga moja linaweza kubeba ndoo saba na kila ndoo moja siwezi kukosa sh 15,000 na nina vijana ambao huwa wananisaidia kusambaza matunda haya,'' alisema Shauri.

Naye mmoja wa vijana ambaye anasambaza matunda, Omari Yasin alisema biashara hiyo imekuwa ikiwaingizia kipato huku akitoa ushauri kwa vijana wenzake kuwa hali ya kujituma kwani ziko biashara nyingi za kufanya ambazo zinaweza kuwakomboa kiuchumi.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi