loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wizara ya Mifugo, Ardhi kuondoa migogoro

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amemuagiza Katibu Mkuu wizara hiyo anayeshughulikia Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuangalia namna ya kukodisha maeneo ya Ranchi za Taifa kwa wakulima ili kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji.

Amesema ni muda muafaka kwa wizara kuangalia namna wananchi wanavyoweza kutumia maeneo hayo kwa tija badala ya kusubiri wawekezaji ambao baadhi yao wamekuwa wakienda kinyume na makubaliano ya mikataba na kuwafanya wananchi wanaoishi karibu na ranchi za taifa kukosa maeneo kwa ajili ya kufanya shughuli zao za kiuchumi.

 Kwa upande wake, Profesa Ole Gabriel amesema atahakikisha anasimamia maelekezo yaliyotolewa na Waziri Ndaki likiwemo la wawekezaji kulipa madeni ya vitalu walivyokodishwa ili Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) inayomiliki maeneo hayo iweze kujiendesha kibiashara kama moja ya malengo ya kampuni hiyo kupitia maeneo yake.

 Mmoja wa wakulima katika Ranchi ya Usangu iliyopo Wilaya ya Mbarali, Uliya Mahenge amemuomba Waziri Ndaki kuwapatia wakulima maeneo kwenye ranchi za taifa ili waweze kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo huku wakilipa kodi ya serikali ya maeneo hayo watakayokodishwa kama ambavyo wafugaji wanavyopatiwa vitalu kwa ajili ya kufugia mifugo kwenye ranchi hizo.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi