loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri awajia juu wawekezaji waliobadili matumizi ya ardhi

WAZIRI  wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ametoa siku 10 kwa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kubaini na kuwanyang’anya maeneo, wawekezaji waliopatiwa vitalu katika ranchi za taifa ambao wamebadili matumizi ya ardhi kinyume na makubaliano ya mikataba yao.

 Waziri Ndaki amebainisha hayo leo wakati alipotembelea Ranchi ya Usangu iliyopo Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo.

Katika ziara hiyo, Waziri Ndaki amezungumza na baadhi ya wawekezaji, wakulima na wafugaji, ambao wanafanya shughuli zao katika ranchi hiyo na kubaini kuwa baadhi ya wawekezaji waliopatiwa vitalu na NARCO kwa ajili ya kufuga na kulima malisho ya mifugo wamekuwa wakikodisha maeneo hayo kwa wakulima na wafugaji kinyume na mkataba.

 “NARCO siku 10 nadhani zinawatosha kubaini watu wanaojiita wawekezaji, waliobadilisha matumizi ya ardhi ambayo siyo kufuga wala malisho wanyang’anywe maeneo kwa kuwa wameenda kinyume na utaratibu wa mkataba kati yao na NARCO,” amesema Mashimba na kuongeza

“Mimi nitafuatilia, nitapenda kupata taarifa mmepata wangapi na wangapi wamenyang’anywa kwa kuwa wameenda kinyume na utaratibu waliokubaliana.” amesema Ndaki

 Waziri Ndaki amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa baadhi ya wakulima na wafugaji wa Wilaya ya Mbarali kuwa wamekuwa wakikodishwa maeneo ya ranchi hiyo na wawekezaji kwa Sh 20,000  kwa hekari moja kwa ajili ya kilimo na madebe 10 ya nafaka baada ya mavuno kwa kila hekari moja, huku wafugaji wakilipa Sh milioni 2 kwa hekari moja katika kipindi cha miezi minne kwa ajili ya kulisha mifugo yao.

 Amefafanua kuwa mkataba wa NARCO na wawekezaji kwa ajili ya kufugia mifugo na kulima malisho hauruhusu wawekezaji kukodisha eneo kwa mtu mwingine kwa ajili ya shughuli zozote kwa kuwa maeneo ya ranchi za taifa ni mali ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi