loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

13 wanaotuhumiwa kutumia walemavu kushtakiwa

WATU 13 wanaotuhumiwa kuwatumia watu wenye ulemavu kwa kazi ya ombaomba katika maeneo mbalimbali watashtakiwa kwa makosa matano ikiwemo kutakatisha fedha haramu kinyume cha sheria na usafirisha haramu wa binadamu, kushindwa kulipa kodi na kuisababishia seikali hasara.

Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka, Biswalo Mganga kuhusu uamuzi wa kufungua mashtaka katika shauri hilo ulieleza kubaini  watu wenye ulemavu , watoto wadogo na baadhi wakiwa ulemavu wa akili walikuwa wamehifadhiwa katika nyumba za kulala wageni zilizotambulika kwa majina ya Kolini, Madiba na Mbokomu.

Amesema nyumba hizo bubu ni mali ya Sadikiel Metta na zilikutwa na walemavu 23 kati yao wanawake nane, wanaume tisa na watoto sita ambao walikuwa wakitumikishwa katika biashara haramu ya kuomba omba mitaani.

Amesema watuhumiwa waliohusika na uhalifu huo kwa kuwasukuma walemavu kwa kutumia baiskeli maalumu ili kujipatia pesa katika biashara hiyo.

Alitaja mashtaka yanayowakabili ni kujihusisha na Uhalifu wa kupangwa na sheria ya kuzuia makosa ya uhujumu uchumi na uhalifu wa kupangwa (Sura ya 200 ya mwaka 2019), Usafirishaji haramu wa Binadamu kinyume cha sheria ya kuzuia usafirishaji Haramu wa Binadamu namba 6 ya mwaka 2008.

Pia wanatuhumiwa kuisababishia Mamlaka ya serikali hasara kinyume na sheria ya kuziia makosa ya uhujumu uchumi na uhalifu wa kupangwa, utakatishaji fedha haramu kinyume na sheria ya kuzuia Utakatishaji Fedha Haramu (sura 23 Marejeo 2019)

Anaeleza kuwa mnamo Januari mosi mwaka huu majira ya 23:00 usiku katika maeneo ya Tandale, Mtaa wa Pakacha, Polisi ilipokea taarifa ya kuwepo nyumba za kulala wageni zilizohifadhi watu wneye ulemavu kutoka mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita, Morogoro, Kagera na Tabora.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi