loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kiama cha watendaji miradi kichefuchefu ya maji chaja

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema kuwa kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji nchini kitatoa hatima ya baadhi ya viongozi na watendaji wa mamlaka za maji na wakala wa maji vijijini (RUWASA) ambao watashindwa kukamilisha miradi kichefu chefu ambayo imekaa muda mrefu bila kukamilika.

Aweso alisema hayo mjini Kigoma jana alipotembelea mradi mkubwa wa maji katika manispaa ya Kigoma Ujiji na kubainisha kuwa anasikitishwa na utendaji wa bodi hiyo chini ya Mkurugenzi wake, Jones Mbike na kusema kuwa hatasita kuivunja bodi hiyo kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Akizungumza hali ya utekelezaji wa miradi ya maji vijijini mkoani Kigoma alisema kuwa anashangazwa kuona mkoa una miradi mingi ambayo haikamiliki na bado RUWASA na mamlaka za maji zinaibua miradi mingine huku ipo miradi ambayo wameshindwa kuikamilisha.

“Mamlaka ina fedha kwenye akaunti lakini unaambiwa bado mradi unaendelea kusuasua huku sababu zisizo na msingi zinatolewa kuhusu kukwama mwa miradi hiyo, hatutakubali jambo hilo wilaya itakayoshindwa kukamilisha miradi hadi kufikia kilele cha wiki ya maji viongozi na watendaji watakaohusika na kukwama kwa miradi hiyo wataondolewa,”alisema Aweso.

Sambamba na hilo Waziri huyo wa mji amezitaka mamlaka hizo kuwachukulia hatua na kuwaondoa wakandarasi wote ambao watashindwa kutekeleza miradi yao kulingana na mkataba na kwamba kazi hizo zinapaswa kufanywa na mafundi kutoka kwenye maeneo ya mradi.

Akizungumzia mradi wa maji unaotekelezwa manispaa ya Kigoma Waziri Aweso alisema kuwa zipo changamoto ambazo mamlaka na wizara zinasimamia kuhakikisha mradi unakamilika hasa ujenzi wa chanzo ambao unatokana na usanifu unaosababisha kukwama kukamilika kwa mradi.

Pamoja na hilo ameitaka bodi ya Mamlaka ya maji Kigoma Ujiji (KUWASA) kufanya kazi na kutoa motisha kwa watumishi wake waweze kufanya kazi kwa ari na kupeleka huduma kwa wananchi .

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa KUWASA,Jones Mbike alisema kuwa pamoja na kukwama kukamilika kwa mradi wa maji safi Kigoma Ujiji kutokana na kuharibiwa kwa chanzo na mawimbi ya ziwa na kufanyika kwa usanifu upya wa eneo la chanzo, hadi sasa upatikanaji wa maji umefikia asilimia 87 kutoka silimia 30 miaka mitano iliyopita.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Kilumbe Ng’enda alisema kuwa pamoja na changamoto za utekelezaji wa mradi wa maji Kigoma Ujiji bado hali ya upatikanaji wa huduma ni wa kusuasua na hasa kuunganisha wananchi majumbani na kwenye magati ya kuchotea maji

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi