loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Trump bado aweweseka Uchaguzi Mkuu

RAIS anayemaliza muda wake wa Marekani, Donald Trump amesema kwamba hotuba yake ya wiki iliyopita aliyowataka wafuasi wake kuvamia bunge la Congress ilistahili.

Trump alisema ni upuuzi kwa wanachama wa Democrats kufanya juhudi za kumshataki bungeni kwa kuchochea uasi. Trump anayeondoka ofisini Januari 20 mwaka huu wakati rais mteule Joe Biden atakapoapishwa, alisema ‘’Nadhani mchakato huo wa kunishtaki unasababisha hatari kubwa kwa taifa letu na unasababisha hasira kubwa . Sitaki ghasia’’ .

Bunge linatarajiwa kupigia kura leo kifungu cha sheria kuhusu kumshtaki rais huyo. Trump alitoa msimamo wake huo jana alipokuwa akiondoka katika Ikulu kuelekea jimbo la Texas ili kuangalia sehemu moja ya ukuta uliojengwa katika mpaka wa taifa hilo na Mexico.

Ilikuwa mara ya kwanza kwa yeye kuonekana hadharani tangu ghasia za Capitol ambapo takribani watu watano walifariki dunia na wengine kujeruhiwa ikiwemo maofisa wa polisi 60.

Bunge la uwakilishi litapiga kura kumuhoji makamu wa rais Mike Pence kwa kutumia kifungu cha sheria cha 25 kumuondoa rais Trump kutoka ofisini, wazo ambalo Pence anadaiwa kupinga.

Kura hiyo inatarajiwa kugonga mwamba hivyo bunge baadaye litafikiria kutafuta kifungu cha kumshtaki rais Trump kwa kuchochea uasi. Democrats wana idadi kubwa ya wabunge katika bunge la uwakilishi , hivyobasi mashtaka hayo huenda yakaungwa mkono kupitia kura .

Iwapo kura hiyo itapita , Trump atakuwa rais wa kwanza nchini Marekani kushtakiwa mara mbili.

Hata hivyo, kushtakiwa kwake kutasababisha kuondolewa madarakani iwapo thuluthi mbili ya maseneta wataunga mkono kura ya maoni dhidi yake. Akizungumza kuhusu ziara yake katika jimbo la Texas , Trump alipuuza tishio la kumuondoa madarakani kikatiba.

WANACHAMA wa Chama cha Republican nchini ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi