loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Adakwa na Mirungi kwenye gari la kubeba maiti

JESHI la Polisi Mkoani Tanga limemkamata mkazi wa Kimara Jijini Dar es Salaam Simon Pasian Tarimo(37) akiwa amebeba mirungi bunda 1685 ambazo ni sawa na kilogramu 133  ikiwa imehifadhiwa ndani ya jokofu la kuhifadhia maiti.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda amesema gari hilo lilikamatwa jana Januari 12,  saa nane usiku huko kwenye Kijiji cha Manga Kata ya Mkata Tarafa ya Mazingira wilayani Handeni.

Chatanda alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akisafirisha mirungi hiyo akitokea Usangi kuelekea Jijini Dar es Salaam ambapo mbinu iliyotumika ni kuweka mifuko sita aina ya salfeti lenye mirungi  kwenye Jokofu linalotumika kuhifadhia Jeneza lenye maiti wakati wa kusafirisha.

Amesema  askari waliokuwa doria walilishtukia na walipotaka kulisimamisha dereva akataka kukimbia na wakamkimbiza na kufanikiwa kumkamata na walimuhoji sababu za kukimbia akiwa amesimamishwa na Polisi.

Kamanda huyo amesema baada ya hapo Askari walifanya upekuzi kwenye  gari na kukuta kwenye eneo la kuweka mwili kuna mafurushi sita yakiwa yamehifadhiwa mirungi ndani yake na ni eneo ambalo wakati wa kwenda lilikaa Jeneza na wakati wanarudi ndipo walipoweka mirungi.

Kamanda huyo amesema katika mahojiano na dereva huyo alisema baada ya kupelekea mwili  Makanya Usangi wakati wa kurudi njiani eneo ambalo aliwekwa maiti akaaamua kuweka mirungi akiamini kwamba angeweza kusafiri salama asipekuliwe kwa sababu anaamini watanzania hawana utamaduni wa kukagua na kupekua magari ambayo yamebeba maiti.

 Alilitaja gari la kusafirisha  miili ya marehemu ambalo limekamatwa na mirungi hiyo kuwa ni lenye namba za usajili T.569 DSZ aina ya Volvo ambalo ni maalumu kwa kubebea miiili ya marehemu ambalo linamilikiwa na mali ya Nuru Funeral Service iliyopo Jijini Dar es Salaam.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi