loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Magufuli ampongeza Maalim Seif

Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli amempongeza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuridhia kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambapo anaamini kitafuta uhasama wa vyama miongoni mwa mwananchi.

Dk Magufuli amesema hayo leo wilayani Chato mkoani Geita kwenye ziara ya Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi mkoani humo ambapo ameambatana na Makamu wake wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad.
 

“Kuna ndoa zilivunjika kule Pemba kutokana na itikadi ya vyama baada ya uchaguzi lakini baada ya Maalim Seif kuridhia kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa zimerudi hivyo haya mambo ya vyama yasitusumbue sisi kama watanzania tunatakiwa kutanguliza maslahi ya nchi mbele” amesema Dk Magufuli
 

Aidha, Dk Magufuli amemtaka Dk Mwinyi kuendelea na kasi yake ya kutumbua majipu kwa wale wote wanaokwamisha maendeleo ya watu na kumtaka Maalim Seif kumsaidia katika hilo ili wale wote wanaofanya ubadhilifu katika mali za umma wapate kushughulikiwa.

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi