loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watumishi Nane Veta Pwani Wasimamishwa Kazi

WATUMISHI nane wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Pwani, wamesimamishwa kazi kutokana na ukiukwaji wa taratibu katika kutunuku zabuni.

Waliosimamishwa kazi ni Leonard Mwandumbya Mwalimu wa  Umeme, Aibu Issa Mwalimu wa Maabara, Haji Sinani Mwalimu wa majokofu na viyoyozi, David Thobias Mwalimu wa Magari.

Wengine ni Erasto Thomas Mwalimu wa useremala na msimamizi wa ujenzi, Tumaini Magina Mwalimu wa Electronics, Paul  Kimaro Mwalimu wa Engineering Science na Kubri  Mkwanda Ofisa Manunuzi.

Hatua ya kusimamishwa kazi kwa watumishi hao imefikiwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa chuo hicho hivi karibuni na kugundua  kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa kutunuku mafundi ujenzi kupitia ‘force akaunti’ uliosababisha ujenzi wa chuo hicho kuzorota.

 “Kuanzia leo nawasimamisha kazi wote waliokuwa kwenye Kamati ya ujenzi na nawaagiza Takukuru kuwafanyia uchunguzi ili kubaini kilichofanya wakakiuka utaratibu kwa kiwango kikubwa hivi,” amesema Kipanga.

Kamati hiyo ya ujenzi yenye jumla ya watu nane ilimtunuku fundi jamii mmoja aliyejulikana kwa jina la Phillipo Urasi, zabuni ya kujenga majengo 16 kinyume na utaratibu unaotaka fundi mmoja kupewa zabuni ya kujenga jengo moja tu.

Aidha, Kipanga amemsitisha fundi huyo kuendelea na ujenzi na kuagiza wachaguliwe mafundi wengine mara moja kutoka kwenye orodha ya wazabuni waliotuma maombi awali ili kazi iweze kumalizika kwa wakati.

Akisoma taarifa ya ujenzi, Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Pwani, Clara Kibodya amesema kuwa mpaka sasa wameshapokea jumla ya Sh. Bilioni 1.1 na kwamba ujenzi mpaka sasa umefikia asilimia 33 na unatarajiwa kukamilika mwisho wa mwezi Machi mwaka huu.

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi