loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TRUMP: Sitaki Upuuzi

RAIS anayemaliza muda wake wa Marekani, Donald Trump amesema  hotuba yake ya wiki iliyopita aliyowataka wafuasi wake kuvamia bunge la Congress ilistahili.

Trump amesema ni upuuzi kwa wanachama wa Democrats kufanya juhudi za kumshataki bungeni kwa kuchochea uasi. Trump anayeondoka ofisini Januari 20 mwaka huu wakati rais mteule Joe Biden atakapoapishwa, amesema ‘’Nadhani mchakato huo wa kunishtaki unasababisha hatari kubwa kwa taifa letu na unasababisha hasira kubwa . Sitaki ghasia’’ .

Bunge la uwakilishi nchini Marekani leo limepiga kura ya kutokuwa na imani dhidi ya rais Donald Trump kwa kuchochea ghasia zilizosababisha uvamizi wa jumba la bunge la Capitol.

Wabunge 10 wa chama cha Republican walishirikiana na wenzao wa chama cha Democrat wamepiga kura za ndio ya kumshtaki Trump. Wabunge 232 walipiga kura za ndio, huku wabunge 197 wakipinga hatua hiyo

Ni rais wa kwanza katika historia ya Marekani kupigiwa kura ya kutokuwa na imani mara mbili ama kushtakiwa kwa makosa ya uhalifu na bunge hilo la Congress.

Rais Trump ambaye ni mwanachama wa Republican sasa atakabiliwa na kesi katika bunge la seneti ambapo iwapo atapatikana na hatia huenda akapigwa marufuku kushikilia wadhifa wowote wa ofisi ya umma.

foto
Mwandishi: WASHINGTON, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi