loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Cameroon tayari kwa Chan 2021

VIWANJA viwili kati ya vinne vitakavyochezwa mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan 2021) ambavyo vimejengwa hivi karibuni na viwili vya zamani vilivyokarabatiwa, viko tayari kwa michuano hiyo.

Kwa mujibu wa waandaaji, viwanja vyote viko tayari kwa ajili ya mechi za mashindano hayo yatakayoanza kesho hadi Februari 17 nchini Cameroon.

Cameroon iko tayari kwa fainali hizo ambazo ni za sita kufanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009, huku miundombinu ya soka ikipongezwa na Rais wa Caf anayekaimu, Constant Omari baada ya ukaguzi wa viwanja vya mechi, viwanja vya mazoezi na hoteli.

Msafara wa Caf ulioongozwa na Kaimu Katibu Mkuu wake anayeshughulikia soka na maendeleo, Anthony Baffoe ulitembelea miji mitatu ambayo itachezwa mashindano hayo ya Yaoundé, Douala na Limbe.

Kwa Wacameroon sio siri soka ni sawa na dini, Chan inatumika kama majaribio ya kuandaa mashindano hayo makubwa. Viwanja vyenyewe ni sawa na vile ambavyo vinaonekana duniani katika nchi zilizoendelea kisoka.

Viwanja hivi ni vya kisasa zaidi ambavyo vinaweza hata kuandaa mashindano ya Kombe la Dunia.

Hatua maalum za kiusalama zimechukuliwa na serikali kwa kutumia polisi kuhakikisha usalama unakuwapo wakati wote pamoja na nidhamu katika majiji hayo.

Kamati ya maandalizi ya Cameroon imwsema kuwa imefikia hatua ya juu kabisa ya maandalizi, ikiwa ni pamoja na kuandaa mahali muafaka kwa ajili ya waandishi wa habari katika uwanja wa michezo wa Yaoundé.

Wenyeji Cameroon `Simba Wasiofugika’ watafungua dimba kwa kucheza dhidi ya Zimbabwe kwenye Uwanja wa Ahmadou-Ahidjo jijini hapa kuanzia saa 10:00 jioni.

Kundi A Uwanja wa Ahmadou Ahidjo- Yaoundé Cameroon, Zimbabwe, Mali, Burkina Faso Kundi B Japoma Stadium-Douala Libya, Niger, DRC, Congo Kundi C Uwanja wa Douala Morocco, Togo, Rwanda, Uganda Kundi D Uwanja wa Stade Omnisports Zambia, Tanzania, Guinea, Namibia.

MMILIKI na Rais wa klabu ya Mamelod Sundown ya Afrika ...

foto
Mwandishi: YOUNDE, Cameroon

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi