loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uwazi na uwajibikaji sekta ya uziduaji waingiza dola bilioni 3.51

MWENYEKITI wa Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Raslimali za Madini,Mafuta na  Gesi Asilia (TEITI), Ludovick Utouh ameeleza uwazi na uwajibikaji  ulivyoleta mafanikio makubwa katika sekta ya madini.

Alieleza hayo kwenye kikao ambacho TEITI ilikutana na wadau kuhamasisha matumizi ya takwimu katika sekta ya madini kwa kufuata misingi ya uwazi na uwajibikaji kilichofanyika jijini Mwanza.

 Utouh  alisema uwazi na uwajibikaji umewezesha kampuni za uchimbaji na utafiti wa madini, mafuta  na gesi asilia kukusanya zaidi ya dola bilioni 3.51. katika kipindi cha mwaka 2017/18.

Katika kikao hicho kilichofanyika mjini Mwanza, Utouh alisema uwazi na uwajibikaji pia umewezesha kuanzishwa kwa masoko ya madini  na ujenzi wa ukuta wa Mirerani na hivyo kuleta ufanisi katika sekta ya madini  na kuwezesha kukuza pato la taifa.

Naibu Waziri wa Madini, Profesa Shukurani Manya alisema  serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ina dhamira ya dhati ya kuona kuwa sekta ya madini inafanyiwa mabadiliko yatakayo wezesha watanzania wote kushiriki katika usimamizi wa raslimali hiyo ya taifa.

Alishukuru kuwapo kwa utaratibu wa kutolewa kwa ripoti za madini kwani unasaidia wananchi kufahamu kwa  uhakika aina na kiasi cha kodi zinazolipwa na kampuni kwa serikali yao, ikiwa ni pamoja na  gharama za uwekezaji na uzalishaji wake.

“Taarifa hizi zinawezesha wananchi na serikali kufahamu mapato kwa sekta hiyo, kodi na tozo zinazosamehewa, kutolipwa  na kampuni, kulinganisha takwimu za uzalishaji madini, gesi asilia na mafuta,” alisema Manya.               

Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira na Usalama Migodini (SHIREMA) mkoani Shinyanga,  Peter Yusuph alishukuru kuwepo kwa mazingira na uwazi katika sekta ya madini akisema, umewawezesha kuelewana na taasisi za madini wa namna  bora ya kugawana mapato.

Alishukuru kuanzishwa kwa TEITI kwani imewezesha kuwapo kwa  mazingira ya majadiliano yenye tija baina ya kampuni za madini, wananchi na serikali, yenye mazingira ya kunufaika kwa pande zote.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi