loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Taasisi zenye ‘mabaraza mfu’ zatakiwa kuyaunda haraka

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Jenista Mhagama ameagiza taasisi na halmashauri zisizo na mabaraza hai ya wafanyakazi kuyaunda haraka yaweze kutekeleza sera ya ushirikishwaji mahala pa kazi.

Alitoa maagizo hayo alipokuwa akifungua kikao cha Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kilichofanyika juzi jijini Dodoma.

Mhagama alisema mabaraza ya wafanyakazi ni chombo muhimu na chachu ya uhusiano mazuri kati ya waajiri na wafanyakazi kwenye maeneo ya kazi na nguzo kuu katika ushirikishwaji wa wafanyakazi kupitia uwakilishi wao.

"Zipo baadhi ya halmashauri na baadhi ya taasisi ambazo hazifanyi vikao vya mabaraza ya wafanyakazi ipasavyo na Halmashauri nyingine hazijahuisha mabaraza ambayo muda wake umeisha," alisema Mhagama

Kwa mujibu wa waziri, hadi mwishoni mwa Desemba mwaka jana, mabaraza 123 ndiyo yalikuwa hai na 62 hayako hai. “Nichukue fursa hii kuziagiza Halmashauri husika kuunda mabaraza hayo na kukaa vikao vya mabaraza kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali na kuhuisha mabaraza hayo," alieleza

Aliongeza kuwa Taasisi zote ambazo hazijaunda mabaraza na ambazo zimeunda kuhuisha mikataba ya mabaraza hayo na kukaa vikao. Pia amezitaka taasisi kutenga bajeti ya utekelezaji wa shughuli za mabaraza kutokana na umuhimu wa mabaraza katika ulimwengu wa kazi. 

Wakati huo huo Waziri Mhagama alikipongeza Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) pamoja na viongozi wa chama hicho kwa kukamilisha ujenzi wa jengo lao binafsi na kununua magari ambayo yatasaidia utekelezaji wa shughuli za chama.

Mwenyekiti wa Talgwu, Tumaini Nyamhokya alisema wafanyakazi wa Serikali za Mitaa pamoja na majukumu makubwa waliyonayo wataendelea kuungana na serikali katika kutatua kero za wananchi kwa kutoa huduma bora wakiongozwa na sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya kazi.

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi