loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Ndumbaro abariki Tawa kujenga soko la samaki Ifakara

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro ameipa baraka  Mamlaka  ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuwajengea soko la samaki  wavuvi wanaofanya shughuli zao katika mto Kilombero.

Pia ametaka kuwekwa kwa usimamizi  endelevu  wa kulinda hifadhi ya mazingira ya bonde  la  Kilombero .

Alitoa baraka kwa Kaimu Kamishna wa Tawa ,Mabula Nyanda , hivi karibuni  Mjini Ifakara,  wilaya ya Kilombero , mkoani Morogoro kwenye kikao na  viongozi wa Serikali ya wilaya ya Kilombero , watendaji wa wizara hiyo, maofisa wa uhifadhi wa Tawa  pamoja na wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa).

Alisema kitendo cha Tawa kuwasilisha kwake taarifa juu ya kusudio la kujenga soko la kisasa la samaki  mjini Ifakara ni wazi kwamba Serikali haijazuia uvuvi, ila uvuvi uendelee kwa taratibu zinazokubalika.

" Wizara katika kutekeleza Ilani ya Chama CMapinduzi (CCM)  haijazuia uvuvi  katika bonde la mto Kilombero kinachotakiwa kuwe na uvuvi endelevu usio haribu mazingira  kwa vile hilo ni eneo la hifadhi " alisema Dk Ndumbaro.

Alisema wananchi wataendelea kuvua samaki kwa kufuata utaratibu  na maelekezo ya Tawa. 

Hata hivyo waziri alimuagiza Kaimu Kamishna wa Tawa ,Mabula Nyanda kuhakikisha kunakuwepo sehemu maalumu ya kuegesha mitumbwi  pamoja na  ulinzi wa askari wa mamlaka hiyo.

Dk Ndumbaro, pia aliagiza Tawa kuweka utaratibu wa wavuvi kuvua samaki kwa maelekezo  na  waende kuuza  kwenye  soko hilo ili waweze kunufaika na kipaato kutokana na shughuli zao  sambamba na kuiingiza serikali mapato kupitia  sekta ya uvuvi.

Awali ,Mbunge wa Kilombero , Abubakar Assenga, alimuomba Waziri Ndumbaro aridhie kufanyika kwa shughuli za uvuvi katika mto Kilombero kwa vile wavuvi wamekuwa wakivua kwa kufuata sheria na ni hodari katika  utunzaji  wa mazingira ya Bonde la Kilombero .

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Kilombero

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi