loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hadhi ya Kombe la Mapinduzi imeanza kuonekana

MIAKA michache iliyopita kulikuwa na dharau kwa timu za Simba na Yanga kutothamini michezo hiyo na kuichukulia kama bonanza lisilokuwa na faida yoyote licha ya waandaaji kuwathamini na kuwahitaji zaidi.

Dharau hizo huenda ni kwasababu sheria zilizokuwa zimewekwa na wenyeji hazikuwa na makali ya kuwabana.

Ilifikia mahali baadhi walikuwa hawaoni umuhimu wake na kutaka kujitoa kwenye mashindano kwa visingizio vya mashindano waliyokuwa wakikabiliwa ya kimataifa hasa huko nyuma kitendo ambacho kiliwahi kuleta malalamiko makubwa hasa kwa waandaaji.

Kuna wakati mwingine, walikuwa wanasema wanapeleka timu za vijana kuwakilisha kuhofia wachezaji wao muhimu wanaweza kuumia. Ni kama walikuwa wanalazimishwa lakini wao hawapendi.

Walisahau Zanzibar ni sehemu ya Tanzania na timu hizo mbili zina mashabiki wengi huko kwa hiyo kushiriki kwao sio tu makombe bali kunawapa nafasi ya kuendelea kuwavuta mashabiki wengine wapya.

Kitendo hicho hakika kilifanya michuano hiyo kukosa mvuto kwasababu timu hizo pendwa zilikuwa hazichukulii maanani sana na hata zikitolewa ziliona sawa.

Na kwa asilimia kubwa pengine unaweza kusema walioupa umuhimu mchezo huo ndio ambao walichukua kombe mara nyingi lakini waliodharau hakika walishindwa kudumu katika mashindano.

 

Dharau hizo zilisababisha kukosa kombe na hata kusababisha mashabiki wao kulalamika pindi walipokuwa wanatolewa mapema.

Lakini mwaka huu mambo yamekuwa tofauti, nawapongeza waandaaji wa mashindano hakika walijipanga kwa kila kitu na shindano lilikuwa lenye mvuto wa aina yake  ukilinganisha na miaka mingine iliyopita.

Kwanini lilikuwa na mvuto? Ushindani umerejea na timu zote zimeonesha michezo mizuri.

Katika timu tisa zote zilizokuwa zimealikwa zilikuwa vizuri isipokuwa ili kufika hatua muhimu ni lazima wengine watolewe na wengine wasonge mbele.

Ushindani uliongezeka kwasababu timu zilichezesha wachezaji wao wa kikosi cha kwanza sambamba na wale waliokuwa hawapati nafasi ya kucheza na wote walikuwa katika kiwango bora.

Kila timu iliyokuwa inacheza na mwenzake ilionesha umakini kuwa inahitaji matokeo mazuri kusonga mbele.

Licha ya kwamba bingwa haenda popote, lakini kushinda ni heshima na kuonesha ni nani yuko vizuri msimu huu.

Kitu kingine kilichofurahisha timu za Ligi Kuu ambazo ni vinara ziliendelea kuonesha kuwa kumbe hawabahatishi ubora wao upo kila mahali.

Ukitolea mfano Simba na Yanga ndio ambao wanaongoza kwenye ligi na wamecheza fainali, hakika wamecheza soka la kuvutia na kuwa makini kila mmoja akidhihirisha yeye ni mbabe kote.

Shindano limekuwa zuri kwasababu ndio timu zenye mashabiki wengi kuliko nyingine limesaidia kujaza Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Jambo lingine ni kwamba timu hizo hazijakutana muda mrefu pamoja zikiwa kwenye mashindano hayo zaidi ya kwenye ligi pekee.

Mashabiki wa huko walikuwa wanatamani dabi ya timu hizo mbili baada ya miaka mingi mwaka huu imetokea na ni wazi watakuwa wamefurahi kuona timu hizo zikicheza pamoja.

Huenda sasa miaka ijayo shindano hilo linaweza kuwa zuri zaidi ya sasa kutokana na kupokelewa vizuri na kuleta msisimuko kwa mashabiki.

WATANZANIA kama walivyo watu wa mataifa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi