loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Mwinyi aomba aungwe mkono vita ya ufisadi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amewaomba wananchi wa Zanzibar wamuunge mkono katika kutekeleza azma yake ya kuiletea maendeleo Zanzibar sambamba na kupambana na ufisadi.

Alisema hayo katika Msikiti wa Ijumaa Miembeni, Mkoa wa Mjini Magharibi wakati akitoa salamu kwa Waislamu  baada ya kukamilisha sala ya Ijumaa.

Alisema uungwaji mkono pamoja na dua vinahitajika kutokana na wanaofanya hayo kunufaika hivyo wanapozuiwa, watatafuta la kufanya.

Dk Mwinyi alisisitiza kwamba aligombea nafasi hiyo kwa azma ya kuwatumikia wananchi wa Zanzibar ambapo katika kutekeleza hayo yapo mambo ambayo yatafanywa na kuwaudhi watu kwa hivyo, uungwaji mkono unahitajika kwani yatakayofanywa yatawanufaisha wengi.

Alisema kwa hatua zinazochukuliwa hivi sasa maendeleo na mafanikio makubwa yatapatikana kwa sababu mambo muhimu ikiwemo amani na umoja yapo nchini licha ya wachache ambao hawajakubali na hao watazidi kuelimishwa.

Alisema viongozi wa siasa wamehubiri amani na umoja kwa vitendo kwa kuungana na kujenga Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa dhamira ya kuleta umoja katika nchi.

Akisoma hotuba ya Sala ya Ijumaa, Katibu wa Mufti, Sheikh Khalid Ali Mfaume ambaye pia ni Imamu wa msikiti huo, alisema Mwenyezi Mungu anasema waumini wote ni ndugu na vyema ikatafutwa suluhu pale wanapokosana sambamba na kumcha ili wapate kurehemewa.

Mfaume alisema suluhu ni jambo jema na migongano haina neema kwani Mwenyezi Mungu amekuwa akisisitiza umoja huku akieleza wale waliolaaniwa wakiwemo walarushwa, wezi na wabadhirifu. Alisema akitokea kiongozi wa kupambana na hayo ni vyema akaombewa dua.

Wakati huo huo, Dk Mwinyi alifika nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya Tano, Dk. Salmin Amour Juma kwa ajili ya kumjuulia hali na kuzungumza naye.

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi