loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mifugo wakanusha kuwapo kwa vifo vya sangara

KATIBU mkuu wa Wizara ya Uvuvi na Mifugo, Dk Rashid Tamatamah amekanusha kuwepo kwa vifo vya  samaki aina ya sangara. Taarifa ya kuwepo kwa vifo hivyo ilitolewa na wavuvi wa maeneo ya  Masonga-Sota wilayani Tarime mkoani Mara.

Alisema Baada ya kupata taarifa kuhusu vifo hivyo, Wizara yake pamoja na Taasisi yake ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) kituo cha Mwanza walifanya ufuatiliaji na kugundua  upande wa Tanzania  vifo vya samaki hao havijaripotiwa sehemu yoyote isipokuwa eneo la wakazi wa Masonga-sota, Tarime walidai kuona vifo hivyo Januari 2 mwaka huu.

“Mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu ilitolewa taarifa ya vifo vya samaki aina ya sangara katika ziwa Victoria nchini Uganda hasa katika maeneo ya Kaskazini magharibi ya nchi hiyo. Samaki waliokufa katika tukio hilo ni aina ya sangara wakubwa,” alisema Tamatamah.

Dk Tamatamah alisema maeneo mengine ya ziwa Viktoria upande wa Tanzania hakuna na taarifa hizo na kuongeza kuwa maeneo hayo ni Malehe mpakani na Uganda, Bukoba, Misenyi, Visiwa vya Ukerewe na Gozba, Busekela-Musoma, Nyamikoma-Busega, Mwanza na Muleba.

Alisema walithibitishiwa na idara ya Uvuvi ya Uganda kuwa samaki waliokufa hawakuwa na sumu   na inadhaniwa vifo hivyo vimetokana na tukio la kila mwaka linalotokana na mchanganyiko wa maji ziwani kati ya tabaka la chini lenye hewa ndogo ya oksijeni na lile tabaka la juu.

Dk Tamahtama alisema vifo hivyo havijaonekana  upande wa Tanzania kuna uwezekana kuwa mchanganyiko wa maji unaweza kutokea kwetu pia kama hali ya hewa itaruhusu wakati wa mvua kubwa na upepo,

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi