loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Magereza waokoa Bil 11/- kwa kujitegemea chakula

JESHI la Magereza nchini limeokoa jumla ya Sh Bilioni 11, ikiwa ni gharama ya chakula cha wafungwa tangu lianze kujitegemea ikiwa  ni maelekezo ya Rais  John  Magufuli ya kulitaka jeshi hilo litumie nguvu kazi ya wafungwa ilionao kuzalisha chakula.

Akizungumza jana katika ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ,iliyofanyika katika Makao Makuu Mapya ya Jeshi hilo ,Msalato jijini Dodoma, Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee alisema walikuwa wanatumia Sh bilioni moja kila mwezi kulipa wazabuni wa chakula waliokuwa wanaliuzia chakula  jeshi hilo.

“Sasa hivi tunajitegemea asilimia kubwa kwa chakula, serikali kabla ya mwezi wa tatu mwaka jana kila mwezi kulikua kuna deni la Sh bilioni moja, lakini baada ya mwezi huo wa tatu sasa tunaokoa kiasi hicho cha fedha Sh bilioni moja na mpaka sasa tuna 12  tunajilisha wenyewe kupitia shirika la magereza,”  alisema Mzee.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Naibu Waziri, Khamis Hamza Chilo alilipongeza Jeshi la Magereza kwa kutekeleza vyema agizo la Rais Magufuli ikiwa sambamba na ujengaji wa kiwanda kikubwa cha samani ambapo mpaka kukamilika kwake kitagharimu shilingi 1,101,743,123/=

“Niwapongeze kwa hatua mbalimbali za maendeleo ambazo zingine nimeshuhudia mwenyewe, lakini kubwa kuweza kujitegemea kwa chakula cha wafungwa hali iliyopelekea kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kinabaki humu humu ndani na mnakitumia kwa shughuli zingine za maendeleo hongereni sana,” alisema Naibu Waziri Chilo.

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi