loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ahimiza maandiko zaidi wahitimu kusaidia jamii

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo amesema serikali ina deni kubwa la kuhakikisha wahitimu wa elimu ya juu wanaomaliza wanasaidia jamii na nchi kwa ujumla katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda.

Akwilapo alisema hayo wakati akifungua kikao cha wadau cha kujadili rasimu ya miongozo ya usalama wa mazingira na jamii katika utekelezaji wa Mradi wa kuboresha elimu ya Juu wa mabadiliko ya kiuchumi (HEET) nchini.

Akinukuu Ilani ya CCM ibara ya 80 alisema, inaagiza kuongeza rasilimali watu katika taasisi za elimu ya juu ikijumuisha wahadhiri hivyo mradi huo umekusudia kusomesha wanataaluma 639 katika ngazi ya umahiri na uzamivu.

“Hii ni fursa kubwa nendeni msimamie walengwa wapate udahili kwa wakati na wamalize masomo yao mapema ndani ya miaka mitano ya uhai wa mradi huo,”alisema.

Katibu Mkuu huyo alisema pia ilani hiyo inaagiza kuboresha na kuongeza miundombinu na vifaa vya kutekeleza kujifunza, kufundisha na kutafiti kwa lengo la kuongeza uwezo wa taifa katika kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi.

“Tayari maandiko yenu ya University Strategic Investment Plan ndani ya mradi huu wa HEET yameorodhesha na naagiza hili litekelezwa vizuri. Aidha nje ya HEET  Vyuo Vyetu vikuu viendelee kuandika maandiko,” alisema.

Pia alisema mitaala yote sasa ilenge soko la ajira na uchumi wa kati, vyuo vikuu hapa nchini vijivunie ni wangapi wameajirika kwani  wazazi wanajitahidi kukopa  ili wawilipie watoto wao gharama za vyuo vikuu wakijua kuwa mtaala ni mzuri.

“Hii ni kero namba moja ya Serikali ya Awamu ya Tano katika wizara yetu. Ikibidi basi muanze kuwaandaa kujiajiri kisaikolojia na kimtazamo kwa fani zote. Msibwage tu huu mzigo kwa serikali,” alisema.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma) katika Chuo Kikuu Mzumbe mkoani Morogoro, Profesa Ganka Nyamsogoro alisema wizara inatambua elimu ya juu inaweza ikaleta mageuzi kiuchumi, mradi hauwezi kwenda bila kushirikisha wadau kwa kuwa  ushiriki wa wadau utasaidia umiliki wa mradi huo.

Alisema wadau wanaahidi kuwa sehemu ya utekelezaji wa mradi huo kama ambavyo imeelekezwa ikiwa ni pamoja na kuongeza rasilimali watu kwenye maeneo yenye uhitaji pamoja na kutoa wahitimu walioiva kuendana na mahitaji ya soko ili kuleta mageuzi ya kiuchumi sambamba na maendeleo ya teknolojia.

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi